TAHADHARI KUTOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA imewataka watumiaji wa taarifa za hali ya hewa katika sekta mbali mbali ikiwemo wakulima,wajenzi,wafugaji mamlaka za wanyama pori,mamlaka za maji na afya kuchukua hatua stahiki katika kupunguza athari mbaya zinazoweza kujitokeza katika msimu wa mvua za vuli unaotarajia kuanza mwezi Oktoba hadi Disemba 2017
Akizungumza na wandishi wa habari Leo jiji dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi amesema mvua za Vuli zinatarajiwa kuanza Septemba, 2017 katika maeneo mengi ya Ziwa Viktoria na mwezi Oktoba, katika ukanda wa pwani, na baadaye mwezi Novemba katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki.
Aidha amesema ongezeko la mvua linatarajiwa katika miezi ya Novemba na Disemba, 2017 na hali kadhalika kutakuwa na vipindi virefu vya ukavu kujitokeza zaidi katika mwezi wa Oktoba, 2017 huku kwa upande wa u kanda wa pwani ya kaskazini yani mikoa ya dar es salaam tanga na pwani,Zanzibar na morogoro mvua zinatarajia kuanza kati ya wiki ya kwanza na ya piliktoba
Msimu wa mvua wa Oktoba hadi Disemba (vuli) ni mahususi kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka (Ukanda wa Ziwa Viktoria, nyanda za juu kaskazini mashariki, Pwani ya kaskazini na maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Kigoma) Na TMA inatarajia kutoa utabiri wa mvua katika maeneo mengine ya nchi yaliyosalia mwezi wa Oktoba Mwaka huu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akitoa utabiri wa msimu wa mvua za vuli unaoanza mwezi Oktoba hadi Disemba 2017. Kulia ni Mkurugenzi Matumizi ya Hali ya Hewa, Dk. Ladslaus Chang’a akiwa katika mkutano huo
Post a Comment