TACAIDS KUJA NA TAKWIMU MPYA ZA VIRUS VYA UKIMWI
Kaimu Mkrugenzi Mkuu wa TACAIDS Bw.Jumanne Issango akieleza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa mkutano kuhusu changamoto na mafanikio katika kupambana na ukimwi nchini uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za TACAIDS leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkrugenzi Mkuu wa TACAIDS Bw.Jumanne Issango akieleza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa mkutano kuhusu changamoto na mafanikio katika kupambana na virusi vya ukimwi nchini kulia ni Kaimu Mkurugenzi Muitiko wa kitaifa wa TACAIDS Bi.Audrey Njelekela mkutano uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za TACAIDS leo Jijini Dar es Salaam
Serikali kupitia Tume ya kudhibiti ukimwi nchini (Tacaids) imesema kuwa novemba mwaka huu itatoa hali halisi ya mwenendo wa viashiria vya ukimwi kitaifa ambapo huwa zinatoka kila baada ya miaka minne huku takwimu za mwaka 2011 zikionesha kuwa maambukizi yalipungua kwa 5.3%
Hayo yamebainishwa na Kaimu mkurugenzi wa Tacaids Jumanne Issango wakati akizungumza na wandishi wa habari leo jijini dare s salaam ambapo amesema kuwa kutokana na utafiti wa mwaka 2016/17 takwimu hizo zitakuwa zimejumuisha karibia makundi yote nchini ambapo utafiti wa kipindi hiki umejumuisha kuanzia mtoto umri wa anavyozaliwa na utafiti huo unalenga kupunguza kiwango cha maabukizi mapya ya vvu kutoka 0.32%mwaka 2012 hadi 0.16% ifikapo mwaka 2018
Aidha amesema kuwa bado kuna changamoto kadhaa katika kudhibiti maambukizi ya virusi vya ukimwi katika makundi maalumu huku idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi yakilenga Makundi ya wanaofanya biashara ya ngono, maeneo ya wavuvi,wachimba madini, wafungwa na waendesha maroli huku Upungufu wa rasilimali fedha na Unyanyapaa bado ni tatzo miongoni mwa jamii za kitanzania
Kwa upande wake Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Muitikio wa Kitaifa kutoka Tume hiyo Bi. Audrey Njelekela amesema Serikali kupitia TACAIDS inaendelea kufanya jitihada mbalimbali za kukabiliana na janga hilo ikiwemo kuandaa na kutekeleza mikakati madhubuti itakayosaidia kupunguza maambukizi kwa kiasi kikubwa.
TACAIDS ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 22 ya mwaka 2001 kwa lengo la kutoa uongozi wa kimkakati, uratibu na kuimarisha juhudi za wadau wote wanaojishughulisha na kudhibiti UKIMWI nchini.
Na Emanuel Mbatilo Salvahabari
Post a Comment