MEYA DAR ASITISHA MKATABA NA KAMPUNI YA UKUSANYAJI USHURU WA MAEGESHO YA MAGARI
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Meya wa jiji la Dar es Salaam Mh.ISAYA MWAITA CHARLES amesema halmashauri ya jiji imefuatilia kwa karibu utendaji wa kazi wa kampuni ya MWAMKINGA AUCTION MART AND BROKERS kufuatia malalmiko ya wananchi na kujiridhisha kwa ushahidi unaojitosheleza kwamba kampuni hiyo imekuwa ikifanya kazi zake kwa kutozingatia matakwa ya mkataba na kuanzisha migogoro isiyo ya lazima kati ya wananchi na halmashauri hiyo.
Aidha Meya MWITA amesema kuwa kampuni hiyo inapaswa kuondoka kwenye maeneo iliyopangiwa kufanya kazi hiyo na kuhakikisha kwamba katika tarehe ambayo mkataba umesitishwa imekabidhi mashine zote za kukusanyia mapato kwa halmashauri ikiwa katika hali nzuri,kuzitengeneza au kufidia mashine za kukusanya mapato iliyoziharibu.
By Emmanuel mbatilo
Post a Comment