SAMIA ATOA HEKO KWA CHAMA CHA MAJAJI (CMJA)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CMJA) leo Jijini Dar es Salaam. Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Kujenga Mahakama shirikishi, inayowajibika na thabiti kiutendaji”
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akielezea jambo mbele ya washiriki wa mkutano wa wanachama wa Chama cha Majaji na Mahakimu kutoka nchi za Jumuiya ya Madola (CMJA) leo Jijini Dar es Salaam. Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Kujenga Mahakama shirikishi, inayowajibika na thabiti kiutendaji”
Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania Mhe. Jaji Ignas Kitusi akifafanua jambo mbele ya washiriki wa mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CMJA) leo Jijini Dar es Salaam. Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Kujenga Mahakama shirikishi, inayowajibika na thabiti kiutendaji”
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CMJA) Jaji John Rounders wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa chama hicho leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Paramagamba Kabudi. Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Kujenga Mahakama shirikishi, inayowajibika na thabiti kiutendaji”
Kikundi cha sanaa kutoka shule ya Sekondari Jitegemee wakituimbuza katika mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya za Madola (CMJA) leo Jijini Dar es Salaam. Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Kujenga Mahakama shirikishi, inayowajibika na thabiti kiutendaji”
Gavana wa Benki Kuu Tanzania Prof. Benno Ndulu (wa kwanza kushoto) na Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Othman Chande (wa pili) wpamoja na baadhi ya Majaji Wakuu kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya ya Madola akiwemo Jaji Mkuu wa Mahakama ya Juu ya Kenya Jaji Francis Maraga (aliyekaa juu) wakifuatilia mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CMJA) leo Jijini Dar es Salaam. Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Kujenga Mahakama shirikishi, inayowajibika na thabiti kiutendaji”
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wanawake wa Mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CMJA) mara baada ya kufungua mkutano huo leo Jijini Dar es Salaam. Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Kujenga Mahakama shirikishi, inayowajibika na thabiti kiutendaji”
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amekipongeza Chama cha Majaji na Mahakimu wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola (CMJA)kwa mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika kuendeleza na kuimarisha viwango na uhuru wa mahakama na kuendeleza utawala wa sheria na kuifanya jumuiya hiyo kuwa imara zaidi.
Akizungumza mapema leo jijini dare s salaam katika ufunguzi wa mkutano wa Majaji na Mahakimu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli amesema kuwa chama hicho kimeendelea kuchochea na kuimarisha uhuru wa mahakama huku kikijitahidi kuendeleza utawala wa sheria katika nchi za jumuiya ya madola
Aidha samia amesema mhimili wa Mahakama ni kuunga mkono jitihada za serikali katika mapambano ya kuondoa umaskini na rushwa ili kufikia maendeleo ya kweli na kusisisitiza kuwa rushwa huondoa uhuru wa mahakama na hivyo kupoteza utawala wa sheria hna kuwataka washiriki wa mkutano huo kupambana na rushwa katika mahakama ili kuhakikisha haki na maendeleo vinapatikana.
Kwa upande wake raisi wa chama cha majaji na mahakimu nchini bwana Ignas Kitusi amesema kuwa suala la rasilimari fedha bado ni tatizo kwenye nchi za nyingi za afrika huwa azitoshrelezi hasa mahakamani hali iyosababisha baadhi ya huduma kuadhirika
mkutano wa Majaji na Mahakimu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola umehudhuriwa na Majaji Wakuu wa Mahakama, majaji na mahakimu,
Na James Salvatory
Post a Comment