Header Ads

header ad

ECOBANK YAZINDUA NJIA SALAMA YA MALIPO KWA MTANDAO


A
Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki ,Ecobank Tanzania, Mwanaiba Mzee, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa Uzinduzi  huduma ya Malipo kwa njia ya Mtandao, inayayojulikana kama MasterPass na MVISA .Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki  hiyo, Respige  Kimati  na Mkuu wa Kitengo cha wateja wa Reja reja, Ndabu Sware (kushoto).
A
Mkuu wa Kitengo cha wateja wa Reja Reja wa Ecobank Ndabu Lilian Sware (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa Uzinduzi  huduma ya Malipo kwa njia ya Mtandao, inayayojulikana kama MasterPass na MVISA. Kati kati Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki hiyo Mwanaiba Mzee na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki  hiyo, Respige  Kimati.
6A
Ecobank Tanzania Head of Digital Banking Philemon Tesha gestures as he addresses the media after the bank launched a Mobile App – MASTERPASS and MVISA which will be a solution to merchants payment.
0D6A1431
Mkuu wa Kitengo cha wateja wa Reja Reja wa Ecobank Ndabu Lilian wakati wa Uzinduzi  huduma ya Malipo kwa njia ya Mtandao, inayayojulikana kama MasterPass na MVISA. Ecobank Tanzania inakuwa Benki ya kwanza hapa Tanzania kuzindua huduma ya Mobile App ambayo inakuwa ni suluhisho kwa huduma za kifedha.
0D6A1423
Baadhi ya wafanyakazi wa Ecobank Tanzania wakifuatilia kwa umakini wa Uzinduzi  wa huduma ya Malipo kwa njia ya Mtandao, inayayojulikana kama MasterPass na MVISA. Ecobank Tanzania inakuwa Benki ya kwanza hapa Tanzania kuzindua huduma ya Mobile App ambayo inakuwa ni suluhisho kwa huduma za kifedha.

……………………..
Ecobank yaja na suluhisho la kufanya malipo salama kwa njia mtandao kupitia MASTERPASS na MVISA .
Ecobank katika kuendeleza dhamira yake ya kutoa huduma bora na kuwa suluhisho kwenye sekta ya biashara ya huduma za kibenki hapa nchini leo imezindua applikesheni ya simu za mkononi itakayojulikana kama Ecobank Mobile App – MASTERPASS NA MVISA ili kusaidia wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali kufanya Malipo kwa njia rahisi na kwa usalama zaidi mahali popote.
 
Mtanzania yeyote ataweza kutumia teknolojia hii ya mpya ya MASTERPASS QR na MVISA kulipia gharama mbali mbali kwa kutumia simu zao za mkononi kwa kupitisha Quick Response (QR) kwa wauzaji mbalimbali wa bidhaa au watoa huduma ndani na nje ya nchi.
 
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Bi, Mwanahiba Mzee alisema “applikesheni ya Ecobank Mobile App ilizinduliwa Februari mwaka huu lakini kwa sasa imeboreshwa zaidi ili wateja wa Ecobank na wale wasio wateja wa bank hii waweze kutumia applikesheni hii duniani kote”.
 
‘Applikesheni ya Ecobank Mobile App ni njia rahisi ya kujipatia huduma za kibenki ndani ya nchi 33 ambazo Benki yetu inafanya biashara lakini pia unaweza kuitumia ukiwa kokote duniani. Wateja wanaweza kupakua applikesheni Ecobank Mobile App na papo hapo kujifungulia akaunti ya Ecobank kwa njia ya mtandao na kuanza kupata huduma za kibenki kama vile kufanya malipo au kuhamisha fedha bila kutembelea tawi lolote la Benki”, alisema Bi Mzee.
 
“Tunayo furaha kwamba applikesheni yetu ni sulushisho la huduma za haraka za kibenki kupitia mtandao wa simu za mkononi na bado inaendea kuboreshwa  zaidi na zaidi na sasa tunatumia teknolojia ya Masterpass QR na Mvisa kwa kufanya malipo mbali mbali, aliongeza.
 
Bi Mzee aliongeza kuwa Masterpass QR na Mvisa ni njia za mtandao (kidigitali) ambazo humfanya mteja kulipa kwa kadi ya Benki au akaunti zake za benki ambazo pia zimeunganishwa katika mtandao huu kwa kugusisha na kufanya malipo. ‘Hii ni njia ya kutumia simu za mkononi ambapo mnunuzi ataweza kumlipa muuzaji au mtoa huduma yeyote na hivyo  inakuwa ni suluhisho kwa wajasiriamli wadogo, wa kati na wakubwa’, aliongeza Bi Mzee.
 
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi Swere Ndabu alisema “Ili kutumia huduma hii wateja wa Ecobank na wasio wateja wa Ecobank wanatakiwa kupakua Applikesheni ya Ecobank Mobile App kwenye smartphone zao kisha wanajisajili kwa kutumia kadi ya Visa au Master , au kufungua akaunti ya Ecobank Xpress papo hapo na kuanza kufanya miamala ya malipo. Kwa wale ambao ni wateja wanatakiwa kupakua na kuanza kutumia applikesheni kwa kutumia debit card au Ecobank Retail internet banking.”
 
“Kwa kutumia applikesheni hii wakati wa kufanya Malipo, mteja atanufaika kwa kuokoa muda wake na  kupunguza gharama za kutembelea tawi la Benki, ataweza pia kufanya Malipo kwa haraka na kwa usalama zaidi pamoja na kuongeza mauzo kwa vile njia hii itachochea matumizi au manunuzi salama. Vilevile itamsaidia muuzaji sana kwani ni njia rahisi ya kutunza kumbu kumbu za mauzo.” alisema Swere.
 
Swere aliongeza kuwa kwa kutumia applikesheni ya Ecobank Mobile App mteja anaweza akahamisha fedha kwenye akaunti yake ya Ecobank akiwa hapa nchini au nje ya Tanzania, pia ataweza kuhamisha fedha kwenda Benki nyingine hapa nchini au kwenda kwenye kadi za Visa duniani kote na pia kwenye mitandao ya simu za mkononi ya M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money

No comments

Powered by Blogger.