WAUZAJI WA MBOLEA NCHINI WAASWA KUFUATA BEI ILEKEZI ZA MBOLEA
Wito umetolewa kwa wauzaji wa mbolea nchini Kufuata bei elekezi kutoka Mamlaka ya udhibi wa ubora wa mbolea Tanzania kwani kwa sasa bei ya mbolea imepungua bei kwa asilimia 20.
Akizungumza na wandishi wa habari Leo jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Lazaro Kitandu amesema kuwa wafanyabiashara watawajibika kuuza mbolea hiyo kwa bei iliyoelekezwa au chini ya hapo na katika kupanga bei ya mbolea mamlaka imezingatia bei ya mbolea kutoka katika chanzo ,gharama za usafirishaji kutoka nje ya nchi hadi hapa nchini ,tozo mbali mbali ,gharama za usafirishaji ndani ya nchi na faida ya mfanya biashara.
Aidha amesema kuwa wamefanya tathimini ya kujua kiasi cha mbolea iliyoko nchini na kujiridhisha kwamba mbolea iliyopo nchini kwa sasa inatosheleza mahitaji ya nchi hadi mwenzi wa Tisa hivyo mbolea kupitia mfumo wa BPS inatarajiwa kufika tarehe 5-15 Septemba itakuwa imefika kwa wakati muafaka kulingana na mahitaji ya hapa nchini kwa msimu wa kilimi 2017/2018
Post a Comment