KANISA KATOLIKI LAIPIGA JEKI SERIKALI KWENYE MAHABUSU YA WATOTO
Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam leo limekabidhiKisima chenye thamani ya Shilingi Milioni kumi namoja laki saba na themanini (Sh. 11,780,000/=) kwaSerikali ili kutatua tatizo la maji katika Mahabusu ya Watoto iliyoko Upanga jijini Dar es Salaam.
Akiongea katika hafla ya makabidhiano ya Kisimahicho Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo amesema lengokuu la Mchango wa Kanisa katika ujenzi wa Kisimahicho ni kuonesha kuwa Kanisa haliko mbali naSerikali katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa na linashirikiana na serikali katika juhudi zake za kuwaletea wananchi maendeleo bila kujali itikadi za kidini chama au kikabila ili kusudi wanapotokakwenye vituo hivyo watambue wamesaidiwa kutokana na mapenzi mema ya kanisa hilo kwa watuwote.
Naye Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema ujenzi wa kisima hicho umesaidia serikali kupunguzagharama ya kulipia bili ya maji ambayo kwa mwezimmoja serikali ilikuwa inalipa Shilingi laki nne kwaajili ya matumizi ya maji katika mahabusu hiyo na fedha ambazo zimeokolewa na ujenzi wa kisimahicho zitatumika kwa ajili ya kuwakatia Bima ya Afya Watoto wanaozuiliwa katika vituo hivyo ilikuwahakikishia upatikanaji wa matibabu.
I
Wakati huo Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa Kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mwakilishi wa watoto na vijana wainjilishaji mtandaoni Padre Thimotheo Nyasulu amesema kuwa, wameamuakutoa msaada huo baada ya kuona changamoto hiyowalipotembelea kituo hicho Desemba ,2016 kama sehemu ya matendo ya huruma kwa kanisa.
Mahabusu za watoto ni moja kati ya huduma kongwe hapa nchini mahususi kwa kuwahifadhiwatoto walio kinzana na Sheria na ambao kwa sababumoja au nyingine hawakuweza kupata dhamana kwakesi au mashauri ambayo yanawakabili Mahakamani.
Post a Comment