MAWAKALA WA FORODHA WAPIGWA MARUFUKU HILI NA SERIKALI SOMA HAPA KUJUA
Serikali imewapiga marufuku mawakala wa forodha wanaogushi nyaraka kwa ajili ya kuingiza kemikali kinyume cha Sheria na pia wanaipotezea Serikali mapato.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Prof. Samwel Manyele wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uingizwaji wa kemikali nchini kutoka nje ya nchi ambapo amesema kwa mujibu wa Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Kemikali nchini kila anayeingiza kemikali anatakiwa awe amesajiliwa na kupewa hati ya usajili huo vile vile anatakiwa kupata idhini ya wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kabla ya kuagiza mzigo wa kemikali nchini.
Aidha Prof. Manyele amesema kuwa lugha elekezi zinazotakiwa kutumika katikakuweka lebo za kemikali husika kuwa ni Kiswahili na Kingereza tu hivyo hakunakemikali itakayoruhusiwa kuingia nchini ikiwa lugha tofauti na hizo
.
Ofisi ya Mkemia Mkuu inaendelea kukabiliana na changamoto za wadau wa kemikali kwa kuendelea kuwaelimisha wadau kuhusiana na matakwa ya Sheria na Kanuni za uingizaji wa kemikali nchini na kuchukua hatua za kisheria kwa wale wanaokiuka matakwa ya Sheria na kanuni zake, kuboresha mifumo, vifaa na sehemu za kufanyia kazi .
Post a Comment