Header Ads

header ad

ZIARA YA RAIS MAGUFULI ITIGI, MKOANI SINGIDA


1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuzindua barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa Kilomita 89.3 mapema leo, kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Makame  Mbarawa na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi.

2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Itigi mara baada ya kuzungumza nao na kuzindua barabara Manyoni-Itigi-Chaya, ambapo pamoja na mambo mengine ameagiza ujenzi wa barabara ya Chaya-Nyaua yenye kilomita 85 na ujenzi uanze ndani ya siku 45 ili barabara hiyo ikamilike kwa kiwango cha lami.
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na umati wa wakazi wa Itigi waliojitokeza kumlaki na kushuhudia uzinduzi wa barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya, Rais Magufuli amewataka wana Itigi kutumia fursa ya kuwa jirani na Makao makuu ya nchi kwa kufanya kazi kwa bidii na kuzalisha bidhaa ambazo zitauzwa huko Dodoma.
4
Umati wa wakazi wa Itigi waliojitokeza kumlaki Rais Magufuli na kushuhudia uzinduzi wa barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya, wakazi hao wamempongeza na kumshukuru Rais Magufuli kwa kuwajengea barabara hiyo ambayo ni muhimu kwa kuwaunganisha na mikoa ya Tabora na Kigoma.
5
Sehemu ya barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya ambayo imezinduliwa leo na Rais Magufuli, Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 89.3 kwa kiwango cha lami imefungua fursa ya usafirishaji kwa urahisi kutoka kanda ya Kati yaani Singida na Dodoma Kuelekea mikoa ya Tabora na Kigoma hadi nchi za jirani za Burundi na Kongo.
6
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa akimkaribisha Rais Magufuli azungumze na wananchi wa Itigi, ambapo amesema barabara ya Manyoni Itigi Chaya imegharimu shilingi bilioni 114.692 na kiunganishi cha Mikoa ya Singida, Tabora na Kigoma kuelekea Makao makuu ya Nchi yaani Dodoma.
1 (3)
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili eneo la Njiapanda Itigi, alipozungumza na wananchi wa eneo hilo na kuzindua barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya.
8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi kwenye eneo la mkutano wa hadhara mara baada ya kuwasili eneo la Njiapanda Itigi, alipozungumza na wananchi wa eneo hilo na kuzindua barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya.
10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amkimsikiliza kwa makini Mhandisi wa TANROADS mkoa wa Singida Leonard Kapongo mapema leo. Katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Itigi, Rais Magufuli amemuagiza Meneja huyo na Wizara ya ujenzi kupitia upya gharama za ujenzi wa barabara ya Itigi Makongorosi yenye urefu wa kilomita 57 ambapo gharama za ujenzi wa barabara hiyo ni bilioni 104.

No comments

Powered by Blogger.