Header Ads

header ad

MAKONDA ATENGUA NAFASI ZA MAAFISA ELIMU 12

kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ametengua nafasi za maafisa elimu kata 12 kutoka katika kata ,mbali mbali zilizopo jijini Dar es salaam.




Mkuu wa mkoa amefanya maamuzi hayo hivi punde baada ya kufanya mkutano na wakuu wa shule za sekondari,waalimu wakuu na maafisa elimu kata hii leo.

Chanzo cha kuwasimamisha nafasi zao ni kutokana na kudai malipo ya posho zaidi na wao wanavyopewa hivi sasa ya kima cha shilingi laki mbili na nusu, fedha kwaajili ya posho ikiwa ni nje ya mishahara yao lakini wamelalamikia mbele ya mkuu wa mkoa kuwa Haziwatoshi katika kufanya shuhuli zao za kimaendeleo ya elimu kwa kata zao .

jambo ambalo lilipelekea kutofautiana baina ya maafisa elimu kata hao ambao jumla ya idadi yao ni 28 lakini hao 12 kati yao walikataa wakitaka kuongezewa kwa posho hiyo.

Hata hivyo Rc makonda amemwagiza Afisa elimu wa mkoa kuwavua vyeo vyao wote 12 na kuwapangia majukumu mengine kisha afanye utaratibu wa kujaza nafasi zao kwa haraka.

"Afisa nakuagiza hawa 12 wote washushwe vyeo vyao pamoja na kuwatafutia adhabu nyingine zaidi,serikali hii ya awamu ya tano haina fedha za kuwapa posho za kiti cha madaraka tofauti na wanazo pewa kwa sasa,tafadhali nenda kawapange wakawe waalimu wa kawaida kwenye shule ambazo zina uhaba wa waalimu"Alisema Makonda

No comments

Powered by Blogger.