VIONGOZI ILALA WACHUKULIENI HATUA KALI WANANCHI WANAOKAIDI MAAGIZO YA SERIKALI "MPINA"
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amewataka viongozi wilaya ya Ilala kuwachukulia hatua kali watu wanaokaidi kutunza mazingira yanayowazunguka.
Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akishiriki katika zoezi la usafi wa kila mwisho wa mwezi.
Amesema kuwa ili kuweza kuhakikisha zoezi hilo linatimia na kuwashirikisha wananchi wote, ni lazima viongozi wawachukulie hatua kali wananchi ambao wanakaidi kushiriki katika zoezi hilo kwa lipo kwaajili ya kuiokoa jamii na magonjwa mbalimbali ya mlipuko.
“Ninyi viongozi mnatakiwa kuwachukulia hatua kali wale wananchi wachache wanaokaidi kushiriki katika usafi, kwani haiwezekani watu wailaumu Serikali kwa kila kitu, sisi viongozi wa juu tuleteeni wale walioshindikana ili tuweze kuwashughulikia,”amesema Luhaga.
Aidha, katika hatua nyingine, Luhaga amewataka wananchi kuunga mkono hatua za zinazochuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwani anania ya dhati kuleta maendeleo ya nchi.
Hata hivyo, pamoja na hayo, Mpina ameongeza kuwa katika awamu hii ya TanoTanzania imepata Rais wa kipekee ambaye amekuwa mfano wa kuigwa barani Afrika na duniani kote.
Wafanyakazi wa kampuni ya kajenjere wakiendelea na Usafi mapema leo
Post a Comment