Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Esnath Magoti akizungumzia matukio ya ukatili ambayo yapo Mkoani Humo.
Na Joel Maduka wa Maduka Online.
Vitendo vya ukatili dhidi ya watoto bado vimeendelea kushamiri Mkoani Geita ambapo Kuanzia mwezi Januari hadi Juni mwaka Huu Jumla ya makosa ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto mia moja Tisini na Tisa (199) vimekwisha ripotiwa kwenye dawati la Jinsia na Watoto.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ofisi za polisi Mkoani Humo,Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Esnath Magoti ,amefafanua kuwa mchanganuo wa Makosa hayo ni kesi za ubakaji,ulawiti ,watoto kutelekezwa ,wengine kutokuwapeleka shule na vitendo vingine vya ukatili dhidi ya watoto.
“Unyanyasaji wa Kijinsia bado ni tatizo kubwa sana kwenye Mkoa wetu wa Geita kwani hadi sasa Jumla ya Kesi mia moja Tisini na Tisa (199) zimekwisha Kufika kwenye meza yetu na kesi nyingi unakuta ni za ubakaji ,ulawiti na wengine wanatenda ukatili wa kuwadhuru watoto mara nyingi kesi hizi zinakwama kutokana na jamii kushindwa kuwa na ushirikiano kwa kutoa taarifa wengine wamekuwa wakimalizana wao kwa wao kwenye familia zao hali hii inakwamisha sana jitihada za utetezi wa watoto ambao wanafanyiwa vitendo vya ukatili”Alisema Magoti.
Hata hivyo kutokana na juhudi za utoaji wa elimu juu ya watu kuachana na vitendo vya ukatili hali bado sio swari ambapo kwenye mtaa wa Msalala Road kata ya Kalangalala,Mama wa kufikia ambaye anajulikana kwa jina la Benitha Augustine,amemchoma mtoto mwenye umri wa miaka minane (8) sehemu mbali mbali za mwili wake na kijiko ambacho alikuwa amekipasha moto kwa madai kuwa alikuwa akimhadhibu .
Akizungumza na Mtandao wa Maduka Online Jirani wa Mama Huyo Bi,Habiba Rajabu alisema kuwa Mama Huyo amekuwa na tabia ya kumpiga mara kwa mara mtoto huyo bila sababu hali ambayo wao kama majirani wamekuwa wakijiuliza labda kwasababu sio mtoto wake wa kuzaa ndio maana amekuwa akimsulubu kwa mateso ya namna hiyo.
“Sisi kama majirani tumeendelea kumshauri kama mtoto amemshinda ni bora akampeleka kwa mama yake kuliko kuendelea kumfanyia vitendo vya ukatili wa namna hiyo amefikia hatua hadi anamchoma na kijiko ambacho amekipasha moto kiukweli inaumaa sana kwa mtoto ambaye ni kiumbe wa Mungu kufanyiwa ukatili wa namna hii yani hadi na baba yake mzazi ana mapenzi na mtoto ukimkuta anamwadhibu utadhani anaadhibu jambazi jamani watu tubadilike ukatili wa jinsi hii haukubaliki kwenye jamii zetu”Alisema Bi Habiba.
Aidha mama Huyo Bi,Benitha Agustine amekiri kufanya kitendo cha kumpiga mwanae na kumchoma kwa kutumia kijiko ambacho amekichemsha kwenye moto na kwamba amekuwa akifanya hivyo kutokana na hasira ambazo zinasababishwa na ugomvi baina yake na mume wake kwani amekuwa akimpiga mara kwa mara hali ambayo imekuwa ikipelekea kupatwa na hasira ambazo zimekuwa zinapelekea kumwadhibu mtoto wake.
Kutokana na kufanyiwa ukatili huo Mtoto huyo ameiomba serikali kumchukulia hatua za kisheria mama yake wa kambo kwani imekuwa ni destulri yake kumtesa kwa muda mrefu hali ambayo imemsababishia kuwa na majeraha sehemu nyingi za mwili wake.
Shida Mpondi ni Katibu wa Mbunge wa viti maalum Chadema Mkoani Hapa ametoa wito kwa wazazi,walenzi na baadhi ya watu wenye tabia za namna hiyo kuachana nazo kwani zinawakosesha haki za msingi watoto na kuwafanya kudumaa kiakili.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
|
Post a Comment