Header Ads

header ad

MIFUKO YA PLASTIC KUPATIWA UFUMBUZI


1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifungua Kikao cha Wazi cha kupokea maoni ya wadau kuhusu dhamira ya Serikali kupiga marufuku uzalishaji,uuzaji,usambazaji na
matumizi ya mifuko ya plastiki leo Jijini Dar es Salaam.
2
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustine Kamuzora akiongea wakati wa ufunguzi wa Kikao hicho leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.
3
Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard  Muyungi akiongea wakati wa Kikao hicho mapema leo.
4
Mwenyekiti wa Umoja wa wazalishaji wa mifuko isiyo na athari kwa mazingira Bw. Jumanne Mgude akionesha mfuko unaozalishwa hapa nchini usio na athari kwa mazingira wakati wa Kongamano hilo.
5
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Wande Printing and Packaging (T) Ltd Bw. Joseph Wasonga akitoa maoni ya wamiliki wa Viwanda vya Kuzalisha mifuko ya plastiki hapa nchini wakati wa kikao hicho.
6
Katibu wa Umoja wa wazalishaji wa mifuko isiyo na athari kwa mazingira Bw. Sadick Mgonge akitoa maoni ya umoja huo wakati wa Kikao hicho leo.
7
Sehemu ya wadau walioshiriki kikao hicho leo Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mjadala na maoni ya washiriki .
 (Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo)
……

Wadau wa Mazingira  na Wazalishaji wa Mifuko ya Plastiki hapa nchini wameipongeza Serikali kwa kuwakutanisha pamoja ili kujadili kuhusu matumizi ya mifuko ya plastiki na kutoa maoni yao kwa Serikali juu ya kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira.

Akizungumza wakati akifungua  kikao cha wazi cha kupokea maoni ya wadau kuhusu dhamira ya Serikali kupiga marufuku uzalishaji, uuzaji, usambazaji na matumizi ya mifuko ya plastiki, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  Mhe. January Makamba amesema dhamira ya Serikali ni kupata maoni ya wadau na wazalishaji wa mifuko hiyo ili Serikali ifanye tathmini kabla ya kuchukua hatua na kuweka mazingira yatakayowezesha utekelezaji wa Sheria ya Mazingira kwa kila mdau.

Aidha amesema kuwa kuanzia sasa Ofisi yake itashirikiana na wadau katika mambo yote yanayohusu mazingira ili kuongeza tija na kutoa fursa kwa wadau hao kutoa maoni yatakayosaidia katika usimamizi wa Sheria na Kanuni.

Kwa upande wake Naibu Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji wa Plastiki Tanzania Bw.Ahmed Abdallah amepongeza utaratibu huo wa Serikali kuwakutanisha  na wadau.

Nao Gerald simon na Rehema Saidi   ni  wawakilishi wa green  peace foundation  amabaYo ni wadau wa uhifadhi na utunzaji wa mazingira, wamesema wanapinga  mmatumizi ya plasitiki kwani plastic yanachafua mazingira na pia ni hatari kwa afya

Kumekuwa na maoni mbalimbali kuhusu matumizi ya mifuko ya plastiki huku baadhi ya wadau wakidai imekuwa na athari kubwa katika mazingira zikiwemo magonjwa, uharibifu wa miundo mbinu na kuletamabadiliko ya tabia nchi .

N a James Bayachamo-Salvanews
....

No comments

Powered by Blogger.