DEMOKRASI BADO NI TATIZO KATIKA NCHI ZA MAZIWA MAKUU
Imeelezwa kuwa Hali ya Demokrasia na Usalama katika nchi za maziwa makuu siyo ya kuridhisha kutokana na baadhi ya viongozi kuingilia na kujaribu kung’ang’ania madaraka,huku wengine wakifanya marekebisho ya vifungu vya katiba za nchi zao ili kujiongezea mihura ya kuongoza hali inayosababisha migogoro ya kisiasa na kupelekea machafuko
Hayo yamebainishwa leo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Asasi za Kiraia za Maziwa Makuu barani Afrika Bw.Joseph Butiku wakati akizungumza na wanahabari kando ya Mkutano wa Kimataifa wa Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR)ulioanza leo jijini Dar es salaam.
Kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Akina Mama wa Afrika Bi. Eunice Musiime amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kujadili agenda ya uimarishaji wa usalama,na Maendeleo ya nchi wanachama wa maziwa makuu kwa kutekeleza agizo la baraza la usalama la Umoja wa mataifa ,katika kusimamia amani,ulinzi na usalama.
Mkutano huo wa ICGLR,umeyakutanisha majukwaa ya wawakilishi mbalimbali ikiwemo Jukwaa la sekretarieti ,Jukwaa la vijana,Wanawake,Jukwaa la wabunge,ambapo wawakilishi hao wanatoka katika nchi wanachama zipatazo 12 za maziwa makuu
Na James Bayachamo-SalvaHabari
Post a Comment