CHADEMA WANACHOCHEA MGOGORO WETU ILA HAWATATUWEZA " MAGDALENA SAKAYA"
Naibu katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Tanzania bara ,Magdalena Sakaya
amesema kuwa mgogoro uliopo ndani ya chama hicho unachochewa na vyama vingine ikiwemo CHADEMA kutaka kukiua chama hicho Tanzania bara.
Aidha Bi SAKAYA ameituhumu CHADEMA kuendelea kupanga mipango ya kukihujumu chama hicho ikiwemo kuwanunua vijana ili waende kuleta vurugu mahakama kuu ilipokuwa ikisikilizwa katika mahakama kuu ijumaa ya wiki iliyopita.
Akizungumzia suala la CHADEMA kuingilia mgogoro wao kwa kuanzisha operesheni ya kuuondoa upande wa LIPUMBA madarakani Bi MAGDALENA amesema kuwa chama hicho hakitaogopa chochote na kiko imara na wanasubiri kuona mbinu chafu zinazofanywa na Chadema huku akilotaka jeshi la polisi nchini kuchukua hatua dhidi ya Chadema kwa kutoa matamko yanayoashiria uvunjifu wa amani na uchonganishi .
Post a Comment