MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA SEMINA KWA WASTAAFU
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Semina kwa wastaafu watarajiwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
amewaagiza waajira wasiopeleka au kuchelewesha michango ya wanachama
kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii nchini wachukuliwe hatua za kisheria
ili kukomesha tabia hiyo.
Makamu
wa Rais ametoa kauli hiyo 3-June-2017 Jijini Mwanza wakati anafungua
semina ya maisha baada ya kustaafu,fursa ya mafao,uwekezaji
iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kwa
ajili ya wastaafu watarajiwa 450 kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza.
Makamu
wa Rais amesisitiza kuwa waajiri wakichangia kwa mujibu wa sheria
kwenye mifuko hiyo watawezesha wanachama wao kupata mafao kikamilifu na
kwa wakati.
Post a Comment