Mkurugenzi Mtendaji HakiElimu, John Kalage (katikati) akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na uzinduzi wa kampeni maalumu ya kuhamasisha ufanikishaji wa elimu ya mtoto wa kike. Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Tafakari wa HakiElimu uliopo ofisi za taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Programu ya Ujenzi wa Vuguvugu la Harakati ya Kumkomboa Mwanamke kutoka TGNP Mtandao, Grace Kisetu na Mkurugenzi, CAMFED-Tanzania, Lydia Wilbard (kulia) wakiwa katika mkutano huo.TAASISI ya HakiElimu leo kwa kushirikiana na asasi wadau wengine watetezi masuala anuai ya kijamii wamezinduwa kampeni maalumu ya kuhamasisha ufanikishaji wa elimu ya mtoto wa kike, huku ikiiomba Serikali kupitia wizara husika kukamilisha mchakato wa kumruhusu mtoto wa kike aliyepata ujauzito aendelee na masomo baada ya kadhia hiyo. Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo imefanyika leo katika Ofisi za HakiElimu jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanahabari wakiwa katika uzinduzi wa kampeni maalumu ya kuhamasisha ufanikishaji wa elimu ya mtoto wa kike. Baadhi ya wanahabari wakiwa katika uzinduzi wa kampeni maalumu ya kuhamasisha ufanikishaji wa elimu ya mtoto wa kike.
Post a Comment