CUF KUIPELEKA RITA MAHAKAMANI
CUF kuipeleka RITA mahakamani kwa kuisajili 'bodi feki'ya wadhamini wa chama hicho iliyo chini ya ngome ya Prof LIPUMBA.
Katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amesema chama hicho kitaifikisha mahakamani wakala wa usajili wa vizazi na vifo (RITA) na kuwasilisha maombi mahakama kuu kupinga kusikilizwa kwa kesi zilizofunguliwa na chama hicho mpaka ufumbuzi kuhusu suala la bodi ya wadhamini litakapopatiwa ufumbuzi.
Akizungumza na wanahabari leo Dar es salaam Maalim Seif pia amemtuhumu afisa mtendaji Mkuu wa RITA kuwa alipokea maagizo 'kutoka juu' kuisajili bodi aliyoiita feki ya wajumbe wa CUF ambao ni genge la Prof.Lipumba kwa ushirikiano na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kinyume na sheria.
Aidha ameongeza kuwa bodi hiyo mpya 'feki' iliyosajiliwa na RITA pia ina lengo la kumwondoa madarakani katibu Mkuu Huyo sambamba na kuidhibiti kwa ukaribu ofisi ya makao makuu ya chama hicho zilizopo Zanzibar jambo ambalo chama hicho hakiwezi kulikubali.
Post a Comment