Header Ads

header ad

WILAYA YA NYANG'HWALE GEITA YAPATA HATATI SAFI YA KUSAFIRIA

Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale   Mkoani  Geita  imepata hati safi kwa miaka 3 mfululizo  licha  ya  halmashauri hiyo kuwa changa.


Akitoa taarifa hiyo mbele ya kikao cha baraza la madiwani mwenyekiti wa halmashauri hiyo Bw, ALOYS MUSA LUBAMBI amesema kuwa kupata hati safi imewajengea weledi wa kuendelea kuzitatua kero za wananchi.


Amesema halmashauri hiyo imekuwa ikikusanya mapato ya ndani na kubana matumizi yasiyokuwa ya lazima hali iliyowapelekea kupata hati safi  toka kuanza kwa halmashauri hiyo.

Hata hivyo halmashauri  ya Wilaya ya  Nyang’hwale   imeelekeza     nguvu   kusimamia miradi ndani ya kata zake  zote ili kuhimiza wananchi kufanya kazi za kuleta maendeleo ndani ya halmashauri

Na Jacqueline- SalvaNews

No comments

Powered by Blogger.