UMUHIMU WA KINA WATAKIWA KUFANYIKA KATIKA AJENDA YA VIWANDA NA UCHUMI WA KATI NCHINI
Imelezwa kuwa ni muhimu kufanyika utafiti wa kina katika sekta mbalimbali ili kusaidia kufanikisha utekelezaji wa
ajenda ya kitaifa ya Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa kati
Waziri wa Fedha na Mipango ,Dr.Philip Mpango amesema hayo jijini Dar es salaam wakati akizindua wiki ya maonyesho ya Utafiti ambayo imefanywa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam(UDSM),ambapo imeanza rasmi leo na inatarajiwa kufikia kilele chake Mei 12mwaka huu.
Amesema kuwa Ajenda ya serikali ya awamu ya Tano ya Rais Dr.Jonh Magufuli imelenga kufikia Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, hivyo tafiti zinazofanywa na wadau mbalimbali ikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es salaam ziendane na mipango ya serikali.
Aidha Waziri amesisitiza matumizi ya rasilimali kama vile Gesi,Mafuta na Makaa ya Mawe,ambapo Chuo kikuu cha Dar es salaam kimeanzisha kozi za Mafuta na Gesi ili kutia nguvu katika kuelekea Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa Kati.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utafiti na Uchapishaji wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (UDSM) Prof Shukrani Manya amesema kuwa wiki ya utafiti inatoa muda kwa wadau mbalimbali kutoka nje ya Chuo kikuu cha Dar es salaam kuona matokeo ya miradi iliyofanyiwa utafiti.
Miradi zaidi ya sabini itafanyiwa utafiti na Wanafunzi na Walimu wa chuo hicho inaonyeshwa katika wiki ya Utafiti kwa Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa Kati chuoni hapo,ikiwemo miradi ya Kilimo,Umeme,Zana za Kilimo na Viwanda pamoja na Tekno hama nakwamba inaendana na malengo ya serikali.
Na James Bayachamo-Salvanews
Post a Comment