WAVUNJIFU WA SHERIA YA TREIN YA ABILIA KUFUNGWA
Siku Chache Baada ya Baadhi ya Vyombo vya habari kuripoti nakuonesha picha ya Abiria wakiwa wamening’inia kwenye madirisha na milango ya mabaehewa ya Treni ya Pugu-Dar es salaam,leo
Shirika la Reli Nchini(TRL)limeibuka nakusema kuwa hatua hiyo inakiuka sheria na taratibu za usafirishaji wa abiria.
Meneja huduma kwa Abiria wa shirika hilo Idd Mzugu amewambia wanahabari leo jijini Dar es salaam kuwa shirika hilo litawachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kutozwa faini ya shilingi elfu hamsini au kufungwa jela kwa muda wa miezi sita wanaofanya vitendo hivyo mujibu wa sheria
.
Amesema kuwa hali hiyo imetokana na kuongezeka kwa idadi ya abiria wakati wa msimu huu wa mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam kutokana na abiria wengi kuacha kupanda magari ya daladala kwa kuhofia foleni barabarani.
Hata hivyo amebainisha Kuwa shirika hilo tayari linampango wa kuboresha sekta hiyo muhimu kwa kuagiza treni za kisasa ambazo zitakuwa na uwezo wa kukimbia kwa kasi hali ambayo itasaidia kupunguza msongamano wa abiria kwenye stesheni.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Frank Gadau ambaye pia ni Mkaguzi wa Polisi kikosi cha Reli amesema kuwa wananchi ambao wamesafiri kwa kuning’inia akiwemo mmoja wa askari polisi wamefanya makosa nakwamba atakayebainika amefanya hivyo adhabu kali itachukuliwa dhidi yake.
Ameendelea kusema kuwa hatua ya abiria kupanda na kuning’inia kweye mabehewa wakati treni inapofika stesheni inatokana na upungufu wa skari polisi kwenye stesheni hizo kwa ajili ya kudhibiti,nakwamba kwa sasa jeshi la Polisi limejipanga kuongeza askari polisi kwenye stesheni hizo.
Post a Comment