Header Ads

header ad

VIJANA MILIONI NNE KUNUFAIKA NA MAFUNZO YA VITENDO'' MAVUNDE"

Vijana zaidi ya Milioni Nne nchini  watafikiwa na 
mafunzo kwa Vitendo ili waweze kuhimili ushindani pindi 
wanapohitimu vyuo.



Akizungumza  leo jijini Dar es salaam  katika  uzinduzi wa mafunzo kwa vitendo  iliyoandaliwa na Chama cha waajiri
nchini (ATE) kwa kushirikiana na Shirika la kazi Duniani (ILO), Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde amesema kuwa Kwenye mafunzo  hayo  ya miaka mitano yanakwenda kuwafikia vijana Milioni Nne nchini ambapo katika mwaka huu wafedha  2017/2018 vijana 27,000 watapewa mafunzo kwa vitendo.


Aidha Waziri Mavunde amewashukuru ATE kwa kuungana na serikali katika kusaidia 
vijana wa kitanzania kuingia katika mpango huo ambao unaondoa pingamizi la kuwataka vijana kuwa na uzoefu hili waajiriwe katika taasisi mbalimbali.


Kwa Upande wake Mkurugenzi mtendaji wa  ATE , Dkt. Aggrey Mlimuka 
amesema mpango huo utawasaidia waajiri kupata wafanyakazi ambao wataweza
kuwasaidia kwa uzalishaji bila ya kuchukua muda mrefu kujifunza.



Na James Bayachamo-salvaNews


No comments

Powered by Blogger.