Header Ads

header ad

LHRC YAITAKA SERIKALI, BUNGE KUREKEBISHA SHERIA YA NDOA ZA UTOTONI


Kituo cha sheria na  haki za binadamu(LHRC), kimeitaka serikali na  bunge kufanyia marekebisho sheria ya ndoa za utotoni ili kumpa mtoto fursa ya kukua na kusoma katika  hali ya usalama  na maadili ili kuweza kuendana  na maisha ya baadae ikiwa ni pamoja na kumuwezesha kupata maisha mazuri hapo baadae.


Haya yasemwa Leo jijini Dar es salaam na jaji mstaafu wa mahakama ya rufaa jaji Eusebia Munuo wakati akizungumza na waandishi wa Habari kwenye uzinduzi wa ripoti ya haki ya binadamu ya mwaka 2016.

Amesema kuwa watoto wamekua wakibebeshwa mzigo mkubwa wa ndoa za  utotoni kitendo kinachopelekea kupata matatizo makubwa yakiwemo vilema pamoja na kushindwa kuwalea watoto.

Aidha  Munuo amewataka wananchi kuachana na vitendo vya kujichukulia sheria mikononi kwa kuwaua vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi kwa imani za kishirikiana.

No comments

Powered by Blogger.