Header Ads

header ad

MWAKYEMBE AWASIHI WANAMICHEZO KUPATA CHANJO YA HOMA YA MANJANO KABLA YA KUSAFIRI.



WAZIRI wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewasihi wanamichezo wa Tanzania wapate chanjo ya homa ya manjano kabla ya kusafiri ili kujikinga dhidi ya ugonjwa wa homa ya manjano  wanapokwenda nchi ambazo zina maambukizi ya ugonjwa huo.


Akizungumza hayo mara baada ya kupata chanjo hiyo katika viwanja vya bunge mjini Dodoma Dkt. Mwakyembe amesema kuwa wanamichezo wanastahili kupata chanjo hiyo ili wasipate ugonjwa pindi wanapotembelea nchi zenye ugonjwa huo.

“Nawaomba wanamichezo na watanzania kwa ujumla wapate chanjo hii ili kusudi wajilinde kutokupata ugonjwa huu kwani tumezungukwa na nchi wanachama ambao wana  ugonjwa wa homa ya manjano” alisema Dkt. Mwakyembe.

Aidha Dkt. Mwakyembe amesema kuwa wanamichezo wanastahili kupata chanjo hiyo kwani huwa wanasafiri mara kwa mara kuwakilisha Taifa  katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas Amesema kuwa  ugonjwa wa homa ya manjano una madhara  hivyo ni vyema kwa wafanyakazi,wafanyabiashara pamoja na  wanafunzi wanaosafiri nje ya nchi hususani nchi zenye ugonjwa huo ni vyema wakajitokeza kupata chanjo.

No comments

Powered by Blogger.