MSAMA ANG'AKA HABARI ZA KUCHAFULIWA YEYE NA FAMILIA YAKE
Mkurugenziwa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi
wa habari ofisini kwake Mtaa wa Mkwepu Posta jijini Dar es salaam wakati
akielezea habari ya gazeti moja la wiki lililoandika habari za kwamba amefilisika
na anatafutwa na mahakama,ikiwemo na kudaiwa kuwakimbia Wafanyakazi wake.
Akizugumza
hayo jijini Dar Es Salaam,Alex Msana amesema yeye ana kampuni nyingi
tu,ambazo zote ni zina Wakurugenzi wake na Mameneja wake,ambao
wanakwenda kwenye shughuli zao za kiofisi kila siku, na Wafanyakazi wapo
na wanaendelea na shughuli zao za kila siku .
"Sijaona mtu
yeyote kutoka Mahakamani akileta ujumbe wa yeye kuitwa mahakamani,
lakini pia hakuna hata taarifa ya yeye kuitwa polisi kwa tuhuma yoyote
kama ilivyodaiwa kwenye hilo gazeti,hivyo habari hizo ni za uzushi na
zinalenga kumpaka matope, lakini baya zaidi zinaihusisha familia yake"
alisema Msama .
Msama amesema kuwa ni kweli amepungunza
Wafanyakazi,hasa katika kitengo cha uchapishaji wa Magazeti,ili kukidhi
hali halisi ya sasa,na kwamba kampuni yake si ya Kwanza kupunguza
Wafanyakazi,anasema kufuatia hatua hiyo amekuwa akisikia maneno na
mengine yakisambazwa kwenye mitandao ya kijamii yenye lengo la kumchafua
yeye pamoja na familia yake.
Amesema
kwa sasa ameamua kuchukua hatau,anajadiliana na wanasheria wake ili
kuchukua hatua za kisheria kuwafikisha mahakamani wahusika, kwa sababu
wamelenga kumvunjia heshima yeye, kampuni zake na familia yake mbele ya
jamii ya Watanzania.
Amesema kuwa mara baada ya kuandaa
utaratibu wa kisheria, watapeleka mashtaka mahakamani ili kudai haki
yake ya msingi ya udhalilishaji uliofanywa na wahusika hao.
Msama
amewaasa Waandishi wa Habari kutumia kalamu zao vizuri sambamba na
weredi wao katika majukumu makubwa ya kuielemisha jamii,katika masuala
muhimu,ikiwemo na kujenga Nchi kwa kila nyanja husika,na si kukaa na
kutunga ama kuzusha habari zisizokuwa na ukweli wowote.

Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akisisitiza jambo wakati
akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusiana na Madai yake
kuchafuliwa yeye na Familia yake kupitia gazeti moja litakalo kwa wiki.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akionesha kukerwa na
habari hizo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye
moja ya ofisi zake jijini Dar es salaam jana
Post a Comment