Header Ads

header ad

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MAFUNZO YA SIKU TATU YA POLISI WANAWAKE KUTOKA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA JIJINI DAR ES SALAAM

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suuluhu
Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya siku tatu ya Polisi
Wanawake kutoka Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika
(SARPCO) kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar es Salaam.

Muonekaniko wa picha kutoka juu ukionyesha Wajumbe wakati wakimsikiliza  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suuluhu
Hassan kwenye ufunguzi wa Mafunzo ya siku tatu ya Polisi
Wanawake kutoka Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika
(SARPCO) kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar es Salaam.
 Mwakilishi Mkazi wa UN nchini, Alvaro Rodriguez akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya siku tatu ya Polisi
Wanawake kutoka Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika
(SARPCO) ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
 Mwaziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya siku tatu ya Polisi
Wanawake kutoka Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika
(SARPCO) kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suuluhu
Hassan akizungumza na Askari wa Kike wa Kikosi cha Kuzuia Fujo (FFU) mara baada ya kufungua Mafunzo ya siku tatu ya Polisi
Wanawake kutoka Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika
(SARPCO) kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar es Salaam.

                        ………………………………………………………………………………….
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka
askari polisi wanawake kutoka kwenye Shirikisho la Majeshi la Polisi Kusini mwa
Afrika (SARPCCO) washiriki
kikamilifu katika oparesheni mbalimbali ambazo zinafanyika kwenye ukanda huo kama
hatua ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu.
 
 

Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli
hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku Tatu ya Polisi wanawake kutoka nchi
wanachama wa SARPCCO katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius
Nyerere Jijini Dar es Salaam.
 
 

Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahimiza askari polisi wanawake kufanya kazi
kwa bidii na kujituma hatua ambayo itasaidia kupanda vyeo kama  askari wanaume katika maeneo yao ya kazi.

Amesisitiza
kuwa muda wa kulalamika kuwa hawapandishwi vyeo umeshapitwa na wakati bali kwa
sasa wachape kazi na waonyeshe kuwa wanaweza majukumu yao wanayopangiwa ili
waweze kupanda vyeo.
 
 

“Vyeo haviji tu ni
lazima polisi wanawake muonyeshe kuwa mnaweza ili muweze kupandishwa vyeo na
kupata nafasi za uongozi katika Majeshi yenu

Kuhusu utendaji
kazi wa Polisi wanawake, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka
polisi hao kutumia mkutano huo wa siku Tatu kujadili kwa kina namna ya kuondoa
changamoto hizo zinazorudisha nyuma utendaji wao wa kazi.
 
 

Amesema kama
polisi wanawake wataacha majungu na kujenga umoja na mshikamano miongoni mwao watafikia
malengo yao haraka hasa katika kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya
vitendo vya uhalifu ikiwemo biashara ya dawa za kulevya.

Kwa upande
wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amesema anaimani kubwa kuwa
mafunzo hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa polisi hao wanawake kuimarika
ipasavyo katika utendaji wao wa kazi.
 
 

Masauni pia
amewahimiza polisi wanawake wanaopata mafunzo hayo kwenda kuwaelimisha na
wenzao mipango na mikakati waliyoweka katika kulinda raia na mali zao katika
nchi zao.

No comments

Powered by Blogger.