WAZAZI WATAKIWA KUWAWEZESHA WATOTO KUTAMBUA CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKTA YA MAZINGIRA
Na James Salvatory- Salvahabari
Wazazi kwa kushirikiana na wadau wamazingira nchini
wametakiwa kuwawezesha watoto kutambua kuwa wana mahusiano na changamoto
mbalimbali zinazoikabili sekta ya mazingira ili waweze kuwa mabalozi
wazuri.
Haya yamesemwa na mratibu wa roots and shoots Bwana
Japhet Mwanango,mbe wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana
na tamasha la watoto lenye kauli mbiu ya wahusishe watu na mazingira
asilia litakalofanyiaka tarehe 22 aprili katika nyumba ya makumbusho ya
taifa
Amesema kuwa wazazi wanapaswa kuwawezesha watoto kutambua
kuwa wana mahusiano na changamoto ya uchafunzi wa mazingira pamoja
kutoweka kwa vyanzo vya maji ili waweze kuwa mabalozi wazuri wa kizazi
kijacho.
Bwana Mwanang,ombe amewataka wazazi kuhudhuria tamashala
la watoto ili kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa na watoto za
utunzaji na uhifadhi wa mazingira,kubadilishana ujuzi pamoja na kutambua
vipaji vya watoto wao.
Naye mkurugenzi, makumbusho na nyumba ya utamaduni Bwana
Achiles Bufere amesema kuwa tamasha hilo litafunguliwa na naibi waziri
wa elimu, sayansi na teknologia Eng Stella Manyanya
Post a Comment