TAARIFA KUTOKA KURUNGENZI YA MAWASILIANO YA RAISI IKULU
Taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu Balozi Kijazi
zinasema Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Kamishna Msaidizi wa Uchimbaji
Mdogo, Mhandisi Benjamin Mchwampaka kuwa Kamishna Mkuu wa Madini.
Kabla ya hapo alikuwa Kamishna Msaidizi wa sehemu ya
uchimbaji mdogo wa madini. Aidha uteuzi wake umeanza tarehe 19 April,
2017.
Wakati huo huo Rais amemteua Adelarnus Kilangi kuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa
Juu wa Petroli(Petrolium Upstream Regulatory Authority - PURA). .
Aidha Bi. Kilangi alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Agustino Tanzania(SAUT) Kampasi ya Arusha. Pia uteuzi wake
umeanza tarehe 19 April, 2017.
Post a Comment