MWENYEKITI WA SOKO LA CHATO AWATAKA WAFANYABIASHARA KUDUMISHA USAFI
Mwenyekiti
wa soko la Chato mjini Bw. Daudi Francisco amewataka wafanya biashara
wa samaki wilayani humo kudumisha usafi katika maeneo yao ya biashara
ili kuepuka magonjwa ya milipuko yanayoweza kujitokeza kutokana na
mvua za masika zinazo endelea kunyesha.
Akizungumza na Maduka online sokoni hapo mwenyekiti huyo amesema kuwa hali ya usafi katika eneo lake inapewa kipaumbele hasa katika kipindi hiki cha mvua za masika ambazo zinaendelea kunyesha.
Aidha
amewataka wafanya biashara wa samaki katika maeneo yanayo zunguka ziwa
victoria kufika katika soko hilo kwa lengo la kujifunza namna ya
kufanya usafi na kuepuka magonjwa ya milipuko yanayo sababishwa na
uchafu.
Kwa
upande wa baadhi ya wafanya biashara katika soko hilo Bi. Zuhura
Benedicto na Mariam Said wamesema kuwa hali ya biashara eneo hilo
imekuwa hairidhishi kutokana na serikali kuweka utaratibu wa kuuza
samaki wenye ukubwa wa kuanzia sentimita 25 hadi 50 sababu inayo
pelekea watu wenye kipato cha chini kushindwa kumudu gharama za kununua
samaki hao.
Sanjari na hayo wafanya biashara hao wa samaki wameiomba Serikali kupunguza vipimo vya ukubwa wa samaki kwani kwa kufanya hivyo itarahisisha biashara hiyo kuwa na mzunguko mkubwa kutokana na samaki hao kununuliwa na watu wa aina zote .
Post a Comment