CHANGAMOTO ZA MUUNGANO ZATATULIWA KWA KIASI KIKUBWA : MAKAMBA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na waandishi wa Habari hawapo pichani juu ya Mafanikio ya Muungano katika kuadhimisha miaka 53 ya Muungano. Kulia ni Mhe. Jenista Mhagama Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akiongea na waandishi wa Habari hawapo pichani juu ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yatakayoadhimishwa katika viwanja vya Jamhuri Mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (kulia) akifuatilia mazungumzo katika mkutano wa waandishi wa habari juu maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano. Kushoto ni Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Baraka Rajab.
…………
Na; Evelyn Mkokoi na Lulu Mussa – Dodoma
Waziri wa Nchi anayeshughulia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba, amesema kuwa changamoto za Muungano wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar zimetatuliwa kwa kiasi kikubwa kutoka 15 mwaka 2006 hadi kufikia changamoto 3 kwaka huu 2017, Muungano unaotimiza miaka 53 wiki ijayo.
Waziri Makamba amezungumza hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa katika mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na waratibu wa sherehe za kitaifa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Walemavu na kusimamiwa na Waziri Mwenye dhamana Mhe Jenista Mhagama.
Mhe. Makamba amezitaja changamoto zilizobakia kuwa ni pamoja na usajili wa vyombo vya moto unaorahisisha kusafirisha magari kutoka Zanzibar kwenda Bara na kutoka Bara kwenda Zanzibar na kusema kuwa swala hili linafanyiwa kazi kwa kumalizwa kwa taratibu za kisheria.
Alisema kuwa changamoto nyingine inahusu Hisa za Zanzibar kwa iliyokuwa bodi ya safari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Pamoja na Mapendekezo ya tume ya Pamoja ya fedha.
Awali akizungumzia Muungano huo unaotimiza miaka 53, Waziri Makamba Alisema kuwa umekuwepo kisheria na umerasimisha udugu na ushirikiano uliyokuwepo kati ya Bara na Visiwani.
Mkutano huo wa waandishi wa habari uliandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Walemavu umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Jordan Rugimbana, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi wa Ofisi hizo.
Post a Comment