Header Ads

header ad

UBALOZI WA NORWAY WAIPATIA UN TANZANIA DOLA MILIONI 5.1 KUFANIKISHA MPANGO WA UNDAP II


Ubalozi wa Norway nchini umeipatia msaada wa dola bilioni 5.1 Umoja wa Mataifa Tanzania ili kusaidia kufanikisha Mpango wa Misaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP II).


Makubaliano hayo yamesainiwa na Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marrie Kaarstad na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez katika ofisi za ubalozi wa Norway uliopo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Balozi Kaarstad alisema msaada huo ni mwendelezo wa misaada ambayo inatolewa na Norway ili kufanikisha mpango wa UNDAP II ambapo kwasasa imefika dola milioni 10.5 na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali na UN katika mpango huo.
,Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marrie Kaarstad akizungumza kuhusu msaada ambao wameutoa kwa Umoja wa Mataifa Tanzania. (Picha zote na Rabi Hume)

"Lengo la msaada huu ni kuwasaidia wakimbizi waliopo Kigoma na kwa wananchi wa Kigoma kwa ujumla, makubaliano mapya tuliyosaini leo yanalenga maeneo yaliyokusudia. Kusaidia kilimo ili kuwezesha kuwepo chakula cha kutosha kwa ajili ya wakimbizi na wananchi wanaozunguka hayo maeneo ya kambi,

"Sehemu nyingine ambayo msaaada huu unalenga, ni kusaidia ni kumaliza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto. Matumaini yetu msaada huu utafungua milango kwa washirika wengine wa maendeleo kuchangia ili kufanikisha mapango huu," alisema

Naye Rodriguez aliushukuru Ubalozi wa Norway kwa msaada waliowapatia na kwa serikali ya Tanzania kwa ushirikiano ambao inautoa kwa Umoja wa Mataifa ili kufanikisha mpango huo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez akizungumza kuhusu msaada ambao wameupokea kutoka Ubalozi wa Norway.

Rodgriguez alisema msaada huo utatumika kama ulivyopangwa kwa wakimbizi na wananchi waliopo mkoa wa Kigoma kwa kuhakikisha kunakuwa na chakula cha kutosha kwa wakimbizi wote wanaokadiriwa kufikia 340,000, lakini pia kuhakikisha kunakuwa na usawa wa kijinsia kwa watu wote.

"Kwa miongo mingi, Norway imeendelea kuwa mshirika wa kuaminika kwa Tanzania na Umoja wa mataifa. Kwa kuweka mkazo katika mahitaji ya wanawake na watoto walio hatarini, rasilimali hizi zitatoa mchango muhimu katika kukidhi mahitaji ya wenye uhitaji mkubwa kama ilivyoelezwa katika Malengo ya Dunia." alisema Rodriguez.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez na Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marrie Kaarstad wakisaini makubaliano ambayo yatawezesha Norway kuongeza dola milioni 5.1 katika makubaliano ya Mpango wa Misaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP II).

No comments

Powered by Blogger.