MHE. MAKALLA ATOA MAAGIZO KWA WATAALAM WA KILIMO
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amepiga marufuku wataalam wa kilimo kukaa ofisini na kwamba ni kinyume cha sheria.
Pia amewaagiza wakurugenzi, wakuu wa wilaya zote mkoani hapa kuhakikisha wanatenga hekta 100 kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda ikiwa ni utekelezaji sera ya uchumi wa viwanda.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla katika akimsikiliza mkazi wa Kijiji cha Kikondo, Joba Chriss baada ya kukagua barabara yenye urefu wa kilometa zaidi ya 200 na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Sekta ya uwekezaji.
"Wataalam wa kilimo ni marufuku kukaa ofisini, sasa ni kuelekeza nguvu kwa wakulima. Kitendo cha kutotekeleza majukumu yao ni kinyume cha sheria,"amesema.
Ametoa agizo hilo leo jijini Mbeya alipokuwa katika mahojiano maalum na matukio360 na kwamba ni lazima maeneo yatengwe ili kuhakikisha serikali inafikia malengo ya kutekeleza uchumi wa viwanda hususan kuwandaa wakulima kuzalisha mazoa yaliyo na tija
"Sera ya viwanda itafikiwa endapo wakulima watakuwa na afya njema na Serikali sasa inawekeza zaidi katika sekta ya kilimo hivyo ni jukumu lenu wakurugenzi, wakuu wa wilaya kusimamia na kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji,"amesema Makalla.
Pia amewaagiza kuweka kipaumbele upatikanaji wa pembejeo kwa wakati, wakulima kupewa elimu ya kilimo kutoka kwa wataalam na si kuwaacha tu.
Makalla, pia amewataka watendaji kuacha mara moja tabia ya
kuwakaimisha maofisa ugani nafasi zao jambo linalosababisha kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavvyo
Post a Comment