LHRC YAOMBA HAYA KWA SERIKALI NA JAMII
Kuelekea siku
ya haki za binadamu duniani inayoadhimishwa Novemba 10 kila mwaka, wadau wa
kutetea haki za binadamu nchini wameitaka jamii pamoja na serikali kuhakikisha
inakomesha vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya siku ya haki za binadamu yaliyoadhimishwa leo Novemba 8, 2017 na kuandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC) , Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bahame Nyanduga amesema tume hiyo inakemea matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yaliyotokea hivi karibuni na kuitaka serikali kukomesha matukio hayo ili nchi isionekane kuwa haiheshimu haki za binadamu.
Aidha, Bahame amevitaka vyombo vya dola kufanyia uchunguzi wa haraka kuhusu matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yaliyotokea, pamoja na mahakama kutenda haki dhidi ya wahusika wa matukio hayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Hellen Kijo-Bisimba amesema serikali inabidi ichukue hatua katika kukomesha matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu ili kulinda haki hizo sambamba na kuifikia jamii yenye haki na usawa.
Naye Balozi wa Swedeni Tanzania, Mama Katarina Rangnitt ameitaka jamii kuendeleza mapambano katika harakati za kutokomeza ukiukwaji wa haki za binadamu, huku akizisisitiza taasisi zinazotetea haki za binadamu kuanzisha midahalo ya wazi yenye lengo la kuibua matukio hayo pamoja na kutoa elimu kwa jamii.
Siku ya haki za binadamu duniani Huadhimishwa Novemba 10 kila mwaka huku kwa Tanzania maadhimisho haya yakitarajiwa kuadhimishwa jumapili hii mjini Dodoma
Na James Salvatory

Post a Comment