Header Ads

header ad

MEYA WA DAR AWAPA ONYO WENYEVITI WA MITAA


NA CHRISTINA MWAGALA,OFISI YA MEYA WA JIJI

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amewataka wenyeviti wa serikali za mitaa kuepuka kujihusisha kwenye suala la uuzwaji wa maeneo yaliyopo mabondeni, yasiyopimwa na yenye migogoro.

Aidha Mwita amewaomba waandishi wa habari kuongoza wananchi katika suala la upandaji wa miti kwenye maeneo wanayoishi.

Mwita amesema kuwa wenyeviti ndio wasimamia wa maeneo hayo na kwamba wanapaswa kujiepusha na mambo hayo kwani kufanya hivyo  ni kujiingiza kwenye migogoro isiyokuwa ya lazima na kuwasababishia wananchi kupata usumbufu wa mafuriko nyakati za mvua.

Kauli ya Meya Mwita imekuja ikiwa ni baada ya kurejea Jijini  hapa akitokea Ujerumani alipokuwa kwenye mkutano wa Mabadiliko ya Tabia ya nchini uliohusisha Mameya wote Duniani, na wataalamu wa masuala ya mabadiliko hayo.

Meya Mwita amefafanua kuwa wenyeviti wa serikali za mitaa ndio wanaosimamia makazi ya wananchi ikiwemo kushugulikia suala la upimaji na kwamba wanalojukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wanaepuka kushiriki katika suala hilo la uuzwaji wa maeneo ambayo yana asili ya mikondo ya maji.

“ Nikweli kumekuwa na migogoro ya namna hii, sasa ni jukumu la kila kiongozi kwenye mtaa wake asikubali kujihusisha kwenye uuzwaji wa maeneo ambayo hayajapimwa, yaliyopo mabondeni, kufanya hivi nikujiletea matatizo kwao na kwa wananchi pia” amesema Meya Mwita.

  Akizungumzia suala la upandaji miti, Meya Mwita amesema kuwa kila mwananchi anapaswa kupanda miti kwenye maeneo wanayoishi na akasisitiza kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kuwa mfano kwenye maeneo yao.

“ Suala la upandaji miti ni jukumu la kila mmoja, lakini katika jiji langu, niwaombe waandishi wa habari muwe mfano kwenye hili ,kwakuwa nyie ndio kikoo cha jamii, iwe upanga, ama umejenga unapaswa kupanda mti kwenye eneo lako” amesisitiza Meya Mwita.

Mwita aliongeza kuwa” hata mimi Meya wenu nimepanda miti kwenye eneo lango, lakini pia nitaendelea kupanda, lakini mtakapounga mkono jambo hili wananchi pia watapata hamasa kubwa kutoka kwenu.

No comments

Powered by Blogger.