Header Ads

header ad

MAELFU YA WAKAZI DAR WAFURIKA KUPATA MATIBABU BURE NDANI YA MELI YA CHINA






Maelfu ya Wananchi wa Dar es Salaam Leo wamejitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa ya Upimaji na Matibabu Bure ndani ya Meli ya Jeshi la Jamuhuri ya China ambapo katika Hali isiyotarajiwa Wananchi kutoka *Mikoani na Nje ya Jumuiya ya Africa Mashariki wamesafiri kuja kufuata huduma hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. PAUL MAKONDA* amewatembelea wananchi hao na kusema *kila atakaefika na kupatiwa kadi atapatiwa vipimo, matibabu na dawa Bure* na kuwaasa wananchi kutimia vyema fursa hiyo.

*RC MAKONDA* amesema Madaktari wengine wa China wanaendelea na huduma za matibabu kwenye *Hospital za Muhimbili, MOI, Ocean Road, Mwananyamala, Amana na Temeke* ili kuhakikisha wanahudumia idadi kubwa ya Wananchi. 

Amesema *hadi kufikia majira ya mchana tayari Wagonjwa 516 walikuwa wamepimwa na kupatiwa Matibabu* jambo linaloonyesha kuwa wananchi wote watapatiwa huduma. 

*MAKONDA* amesema *wapo madaktari bingwa maalumu waliobobea kwa kutoa dawa za kichina* kwa wale wagonjwa ambao dawa nyingine zimekuwa zikishindwa kutibu. 

Amesema lengo ni kuhakikisha *Hakuna mtu anaepoteza maisha kwa kigezo cha kukosa huduma au kumudu gharama.*

No comments

Powered by Blogger.