Header Ads

header ad

JKCI WANATARAJIA KUWAFANYIA UPASUAJI WAGOJWA 18 WA MOYO


dakatati Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Saifee ya nchini India wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) wakati wa kambi maalum ya siku sita ya upasuaji wa moyo inaydaktari  Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Saifee ya nchini India wakiendelea na kazi ya kumfanyia mgonjwa  upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) . Jumla ya wagonjwa 18 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo katika  kambi maalum ya upasuaji wa moyo ya siku inayoendelea katika Taasisi hiyo.
Picha na JKCI
………….
Na Mwandishi wetu

Jumla ya wagonjwa 18 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo katika kambi maalum ya upasuaji inayofanywa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya New Delhi nchini India.


Upasuaji wa moyo unaofanyika katika kambi hiyo ya siku sita ni wa kufungua kifua kwa watu wazima. Upasuaji utakaofanyika ni wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) na kubadili milango miwili hadi mitatu ya  moyo (Valve).

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam  Daktari bingwa wa Moyo na mishipa ya damu ambae pia ni Kaimu mkurugenzi wa Idara ya upasuaji wa Moyo Bashir Nyangasa alisema katika kambi hiyo  wanatarajia kufanya upasuaji kwa wagonjwa watatu kwa siku.

Dkt. Nyangasa alisema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni wagonjwa wengi wanaowapokea mioyo yao kutokuwa katika hali nzuri na hivyo kuwashauri wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara hii itawasaidia kujuwa kama wanamatatizo ya moyo au la na hivyo kupata tiba kwa wakati.

Aidha Dkt. Nyangasa aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia damu kwani wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa moyo wanahitaji kuongezewa damu nyingi.

“Mgonjwa anayefanyiwa upasuaji wa moyo anahitaji damu kati ya chupa 5 hadi 6 hivyo basi tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kwaajili ya kuchangia damu,  hii itasaidia Taasisi kuwa na damu  ya kutosha kwa ajili ya wagonjwa wetu”, alisema.

Alimalizia kwa kuwasihi  wananchi kujiunga na mfuko wa taifa wa bima ya afya ambao utawasaidia kulipa gharama za matibabu pindi  watakapougua na kuhitaji kupata matibabu.

Kambi hiyo inaenda sambamba na utoaji wa elimu ya upasuaji wa moyo pamoja na  kubadilishana ujuzi wa kazi.

No comments

Powered by Blogger.