ZITTO AACHIWA KWA DHAMANA
Mbunge wa
Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameachiwa huru
kwa dhamana na kutakiwa kuripoti siku ya Jumanne saa tatu asubuhi kwa
Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai (DCI) jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria wa
Zitto Kabwe amesema kuwa mpaka sasa mteja wake anatuhumiwa kwa makosa
mawili tofauti likiwepo kuchapisha taarifa kinyume cha sheria ya
mitandao lakini kosa jingine ni kutoa takwimu za uongo kinyume na
kifungu cha 37 (5) cha sheria ya takwimu ya mwaka 2015 hivyo mwanasheria
anasema Zitto Kabwe amehojiwa na kutoa maelezo yake hivyo wanasubiri
kujua kama watakwenda mahakamani.
Kwa upande wake
Zitto Kabwe amefunguka na kusema kwa sasa wanasubiri kuona wanapelekwa
mahakamani ili waweze kujadiliana huko na kusema kama wao kuna makosa
ambayo wanayaona kwake sehemu pekee ambayo wanaweza kwenda kufafanua
vizuri ni mahakamani na kudai kuwa kama asingekamatwa angeshangaa kwa
kuwa tayari Rais alikuwa ameshatoa agizo.
"Tunasubiri ni lini watatupeleka mahakamani kwa
ajili ya kutetea masuala ambayo tumezungumza lakini ya ziada ni kama ambavyo
Mwanasheria amezungumza kwa hapa ni makosa mawili ya Sheria ya Takwimu na
Sheria ya makosa ya mitandao, wananchama waendelee kuwa watulivu tu kwa sababu
kila mtu alitarajia kuwa tutakamatwa kwa kuwa Rais alisema kuwa nikamatwe hivyo
tusingekamatwa ningeshangaa, la ziada ni kwamba tusubiri mahakamani
itakuaje" alisisitiza Zitto Kabwe
Mbali na hilo
kiongozi huyo wa ACT Wazalendo amewataka wanachama pamoja na viongozi wa
chama hicho kuendelea na harakati za uchaguzi mdogo wa udiwani na
kusema endapo wakishinda katika uchaguzi huo ni kitu ambacho kitakuwa
faraja kwao
Post a Comment