Header Ads

header ad

UFAFANUZI JUU YA TUHUMA ZA USHIRIKIANO WA TANZANIA NA KOREA KASKAZINI


Pix 01
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari wakati akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Korea ya Kaskazini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Pix 02
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Korea ya Kaskazini, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Aziz Mlima na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara hiyo Bi. Mindi Kasiga.
Pix 03
Mwandishi wa Habari toka kituo cha Televisheni cha Channel Ten, David Ramadhan akimuuliza swali Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (aliye kaa katikati) wakati Waziri huyo akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Korea ya Kaskazini.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Augustine Mahiga amesema kuwa Tanzania haina uhusiano wowote na Korea ya Kaskazini kama inavyoshutumiwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Septemba 5 mwaka huu, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limewasilisha ripoti katika ofisi za ubalozi wa Tanzania Mjini New-york Marekani,ripoti ambayo imeitaka Tanzania kutoa maelezo juu ya uhusisno uliyopo na Korea kaskazini ambayo imewekewa vikwazo na baraza hilo kutokana na kutengeneza silaha za mangamizi kama vile mabomu ya nyukria.
Mh.Mahiga amesema baada ya kupokea ripoti hiyo tayari amefanya mazungumzo na wawakilishi wa kudumu  wa baraza hilo kutolea ufafaunuzi wa suala hilo,lakini hata hiyvo amedai kuwa serikali inatarajia kuwasilisha ripoti kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya ufafanuzi zaidi kuhusiana na tuhuma hizo.
Amesema kuwa Serikali ya Tanzania inalaani  na itaendelea na msimamo wake wa kupinga utengenezaji wa silaha za mangamizi nakwamba haina uhusiano wowote na korea kaskazini 2014.
Amesema kuwa mazungumzo ya amani yanahitajika ili kupatikana suluhu katika nchi zenye mizozo ikiwemo Japani,Marekani,Korea kusini na Korea Kaskazini na siyo kutumia silaha ambazo zimekuwa zikisababisha athari kubwa kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.
Hata hivyo amewaomba watanzania kuendelea kuwa watulivu huku serikali yao ikichukua hatua nakwamba sula hilo litamalizika kwa amani ,kwani Amani ,Usalama ni sehemu ya Nchi yetu,hivyo Tanzania itaendelea kusimamia msimamo wa kupinga utengenezaji  wa silaha za mangamizi.


No comments

Powered by Blogger.