Header Ads

header ad

SERIKALI YAJIDHATITI KUJENGA VYUMBA VYA UPASUAJI 170 KWA WAJAWAZITO


#1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na waandishi wa habari (Hawapo kwenye picha) mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa tukio la kupokea mashine ya kutoa dawa ya usingizi kutoka kwa taasisi ya Utepe mweupe, pembeni ni Waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu.
#2
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akipokea msaada wa mashine ya kutoa dawa ya usingizi  kutoka kwa Mratibu wa Utepe Mweupe Bi.Rose Mlai wakati wa  tukio lililofanyika mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
#3
Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa tukio la kupokea mashine ya kutoa dawa ya usingizi kutoka kwa taasisi ya Utepe mweupe lililofanyika mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
#4
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiongea na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) wakati wa kupokea msaada wa mashine ya kutoa dawa ya usingizi kutoka kwa taasisi ya Utepe mweupe mapema leo jijini Dar es salaam, pembeni ni Mratibu wa Utepe Mweupe Bi.Rose Mlai.
#5
Mashine ya kutoa dawa ya usingizi (Anesthesia) iliyokabidhiwa kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto  mapema leo jijini Dar es salaam  kutoka kwa  taasisi ya Utepe Mweupe chini ya Mratibu wake Bi.Rose Mlai.

…………………….
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia, Wazee na Watoto imejidhatiti kujenga vyumba vya upasuaji 170 kwa wajawazito ili kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga mpaka kufikia Juni 2018.
Akizungumza hayo wakati wa kupokea mashine ya kutoa dawa ya usingizi Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alisema kuwa ujenzi wa vyumba hivyo vitasaidia kupunguza vifo vya wajawazito kwa asilimia 80  kufika 2025.
“ Si tu vyumba vya upasuaji bali tutaimarisha mahitaji muhimu ikiwemo kujenga maabara ya damu,wadi za wazazi,tutanunua vifaa vyote vya upasuaji na kujenga nyumba moja ya watumishi wa afya kwenye kila kituoa cha kutolea huduma ya afya” alisema Waziri Ummy.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa msaada wa mashine hiyo ya kutoa dawa ya usingizi kutoka  Utepe Mweupe utaisaidia kupambana  kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga kwa asilimia 40 kufikia 2020 nchini.
Aidha Waziri Ummy amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya afya kuongeza wataalamu wa kutoa dawa ya usingizi wakati Serikali ipo katika mkakati wa kuongeza vifaa na dawa kwenye vituo vinavyotolea huduma ya afya hasa uzazi.
“Kama mpaka Juni mwakani tutakuwa tumemaliza hivyo Vyumba 170 vya upasuaji  wa kutoa watoto kwa wajawazito basi Katibu Mkuu na watendaji wako  mnatakiwa kuongeza wataalamu wa kutolea dawa ya usingizi wawili kila kituo kwa hiyo jumla wawe wataalamu 340” alisisitiza Waziri Ummy.
Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imejiongeza kwa kutenga bilioni 8 kwa ajili kununua dawa za uzazi salama  ikiwemo dawa za kuzuia kifafa cha mimba,kuzuia mama kuvuja damu na hupatikana bila ya gharama yoyote.
Mbali na hayo Waziri Ummy amewataka wanawake  kuhudhuria kliniki angalau mara nne kwa mwaka ili kuweza kutambua hali na usalama wa ujauzito na kiumbe kiliochokuwa tumboni kabla ya kujifungua kwa dhumuni la kujifungua salama.
Kwa upande wake mratibu wa Taasisi ya Utepe mweupe Bi. Rose Mlai amesema kuwa mashine hiyo ya kutolea dawa ya usingizi imetolewa na Shirika la Gradians Health kutoka nchini Marekani kupitia Muungano wa Utepe mweupe wa uzazi salama ili kudumisha afya ya mama na mtoto.

No comments

Powered by Blogger.