Header Ads

header ad

DKT.KIGWANGALLA AFUNGUA MKUTANO WA KWANZA ULIOHUSISHA WADAU WA SEKTA YA AFYA YA BINAFSI

# 1
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla akifungua mkutano wakwanza   uliohusisha wadau wa sekta ya Afya ya binafsi na ya umma, uliofanyika mapema leo katika ukumbi wa Banki kuu ya Tanzania jijini Dar es salaam.
# 2(i)
Wadau mbali mbali wa sekta ya Afya ya binafsi na ya umma wakifuatilia mjadala uliofunguliwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla kuhusu masuala ya utoaji wa huduma za Afya nchini Tanzania.
# 3
Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya  Dkt. Dorothy Gwajima akimkabidhi cheti Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa ufunguzi wa mkutano wakwanza  wa wadau wa Sekta ya Afya ya binafsi na ya umma  uliofanyika mapema leo katika ukumbi wa Banki kuu ya Tanzania jijini Dar es salaam.
# 4
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla akigawa cheti kwa mmoja wa wadau kutoka sekta ya Afya ya Binafsi katika mkutano wa ufunguzi  wa kwanza wa wadau wa sekta ya Afya ya binafsi na ya umma uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.
# 5
Meza kuu ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi wakati wa ufunguzi wa mkutano wakwanza   wa wadau wa sekta ya Afya ya binafsi na ya umma, wa kwanza kushoto ni kiongozi Mkuu wa APHTA Dkt. Samwel Ogillo  na wa mwisho kulia  ni Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya  Dkt. Dorothy Gwajima.
# 6
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi wakiteta jambo na Mkuu wa APHTA Dkt. Samwel Ogillo wakati wa ufunguzi wa mkutano wakwanza  wa wadau wa Sekta ya Afya ya binafsi na ya umma ulioongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla mapema leo jijini Dar es salaam.
# 7
Picha ya Pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi wakati wa ufunguzi wa mkutano wakwanza  wa wadau wa Sekta ya Afya ya binafsi na ya umma,kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Coopenation Bi Camilla Christensen, akifuatiwa na  Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya  Dkt. Dorothy Gwajima na wa mwisho ni Mkuu wa APHTA Dkt. Samwel Ogillo.




Sekta ya umma na sekta binafsi zimekutana kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Afya ili kuleta ufanisi kwenye huduma bora za Afya na Ustawi wa jamii hapa nchini.
 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa Afya,maendeleo ya Jamii,jinsia,wazee na watoto Dk.Hamisi Kigwangala amesema kuwa changamoto zilizopo kwa sasa katika sekta hiyo ni ukosefu wa vifaa tiba kwa wingi na kutokuwepo kwa viwanda vya kutosha vya kuzalisha dawa na vifaa tiba hapa nchini.
       Aidha Dk.Kigwangala amesema mjadala huo ambao wamejadili unaweza saidia kukuza na kueneza viwanda vingi nchini vitakazo zalisha dripu,vidonge na vifaa tiba mbalimbali.
          Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa tiba katika wizara ya afya nchini Dk.DOROTHY GWAJIMA  amesema kuwa wamekutana kwenye mkutano huo na kujumuika na sekta mbalimbali za afya nchini ili kujadili mafanikio pamoja na changamoto zinzaoikabili sekta ya afya na vilevile wao kama serikali wanapokuwa wanasimamia huduma za kudhibiti uhusiano pindi tija inapopungua na kuongezeka. Ushirikiano huo utaweza kusaidia kutatua changamoto zilizoko katika sekta hiyo.

No comments

Powered by Blogger.