Header Ads

header ad

UBER IMEZINDUA MIONGOZO YA USALAMA KWA WASAFIRI KATIKA KANDA YA AFRIKA MASHARIKI


uber.png
Dar es Salaam, Tanzania Tarehe 23 Agosti 2017 – Kampuni ya Uber imeanzisha kampeni ya kuhamasisha inayotoa miongozo inayowahimiza watumiaji wa programu hiyo kutumia fursa ya teknolojia ya kampuni hiyo inayoiwezesha Uber kuimarisha usalama miongoni mwa wasafiri na madereva. Miongozo hii ya usalama sasa inapatikana kwa watumiaji wake wote walioko jijini Nairobi, Mombasa, Dar es Salaam, na Kampala.
Miongozo hii ya usalama ni ushahidi wa juhudi za Uber za kubuni teknolojia rahisi na ya uhakika, inayorahisisha shughuli za wasafiri na madereva sambamba na kuwalinda wanapokuwa safarini.
Katika miongozo hii, wasafiri wanaombwa wathibitishe namba za usajili za gari ili wahakikishe zinafanana na gari lililo kwenye programu, kadhalika picha ya dereva kabla ya kupanda  gari. Aidha, madereva wamepewa mafunzo ya usalama, mbali na kwamba wana namba ambazo wanaweza kupiga bure iwapo kuna tatizo.
Meneja Msimamizi wa Uber nchini Tanzania Bw. Alfred Msemo amenukuliwa akisema: “Kampuni ya Uber imekuwa ikitoa usafiri salama na wa kutegemewa na  Watanzania kwa mwaka mmoja sasa. Watu wengi wanategemea Uber katika mahitaji yao ya usafiri kila siku. Uber inatumia teknolojia kuhakikisha kuna usalama katika huduma zetu kuanzia mwanzo hadi mwisho wa safari: kabla ya msafiri kupanda gari, wakati wa safari, na baada ya kuwasili mahali anakoenda.”
Zana hizi za usalama zinawataka wasafiri wasiondoke kwenye programu wakati wa safari kwa sababu safari inafuatiliwa kwa kutumia mfumo wa GPS kuanzia mwanzo hadi mwisho. Ufuatiliaji huu unawawezesha kuona barabara wanayotumia, mahali gari lipo, na kujua iwapo dereva anatumia barabara sahihi. Programu ya Uber pia inatumia kipengele kinachowawezesha wasafiri kutuma maelezo ya safari zao mubashara kwa jamaa na marafiki, ikiwa ni pamoja na barabara wanayotumia na muda wa kuwasili.
Mapema mwaka huu, Uber ilichapisha miongozo ya jamii katika kanda ya Afrika Mashariki, Makala yanayolenga kutoa mwongozo wa tabia ambazo wasafiri na madereva wanapaswa kudumisha na jinsi ya kuchukuliana wao kwa wao wanapokuwa safarini.
Tazama mikakati iliyo hapa chini ambayo wasafiri wanahimizwa kuzingatia:  
Usaidizi wa Ndani ya Programu: Hii ni zana iliyoundwa ili iwasaidie wasafiri kupata jibu haraka wanapouliza swali lolote. Msafiri anaweza kutumia mfumo wa huduma kwa wateja kwa kuenda kwenye sehemu ya “Usaidizi’’ kwenye menyu, zana hii inawasaidia wasafiri na madereva kueleza wasiwasi walionao wakati wa safari na watapata majibu mara moja.
Kuonesha Maelezo ya Safari: Teknolojia ya Uber imefanikisha uwezo wa kufuatilia safari zote kwa kutumia mfumo wa GPS. Abiria akiwa safarini anaweza kufuatilia safari yake katika programu sambamba na kuwaambia jamaa zake Muda Atakaowasili (ETA). Teknolojia hii itawasaidia jamaa na marafiki kufuatilia mahali alipo na wanaweza kufanya hivyo bila kutumia programu ya Uber!
Jua Safari Yako: Wasafiri wanahimizwa watumie vipengele vya usalama vinavyopatikana katika programu, kumbuka kwamba msafiri anaweza tu kuita usafiri wa Uber kwa kutumia programu ya Uber, kwa hiyo watumiaji wasikubali madereva ambao wanajiitia kwamba wanafanya kazi na kampuni ya Uber wawachukue.
Ni muhimu wasafiri wawe wangalifu na wasitumie muda mwingi wakiwa wamesimama wenyewe na simu zao mkononi wanapotaka kuita gari. Wanashauriwa kusubiria ndani ya jengo mpaka programu iwaoneshe kwamba gari limewasili.
Mjue Dereva Wako: Dereva akikubali safari, msafiri anaweza kuona jina, picha, namba pleti, aina ya gari, na rangi ya gari. Maelezo haya yote utayaona kwenye programu – kwenye ramani. Wasafiri wanaombwa wahakikishe kwamba maelezo waliyoona kwenye programu yanawiana na maelezo ya gari kabla ya kupanda..
Fuata Machale Yako: Wasafiri wanaombwa wahakikishe kwamba wanaelewa mazingira yao wanapotumia Uber, ikitokea kwamba kuna kitu chochote wanachokishuku wanaombwa watumie busara kufanya maamuzi yenye tija maishani mwao. Wawe wangalifu wanapoonesha maelezo yao na wahakikishe kwamba wanathibitisha kwamba dereva anayewaendesha ni yule waliyemwona kwenye programu, na kama wanahisi kwamba wanahitaji usaidizi wa dharura, wanaombwa wawasiliane na meza yoyote ya dharura iliyo karibu mara moja.
Toa Maoni: Wasafiri wanaombwa kutoa maoni kuhusu safari ilivyokuwa. Maoni haya yanasaidia kuboresha wigo wa safari za Uber kwa kila mtumiaji, kudumisha huduma za ubora wa hali ya juu na kuleta uwajibikaji. Kampuni ya Uber ina kikosi maalum kinachotoa huduma kwa wateja wakati wowote kote ulimwenguni kinachopitia maoni na kuchukua hatua stahiki kutokana na ripoti na mienendo inayokiuka Miongozo ya Jamii ya Uber.

No comments

Powered by Blogger.