TIC KUANZISHA MFUKO WA BENKI YA ARDHI
Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kinampango wa kuanzisha mfuko wa Benki ya Ardhi ili kusaidia katika kurahisisha upatikananji wa ardhi hiyo katika uwekezaji wa viawanda.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi mtendaji wa TIC Geofrey Mwambe amesema kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa mikakati ya kituo chake kuhakikisha maeneo maalumu ya ujenzi wa viwanda na miradi mingine yanatengwa nchi nzima ili wawekezaji wa ndani na nje wasipate shida wakati wa kuanzisha miradi ya ujenzi wa viwanda
Mwmbe ameendelea kusema kuwa maeneo yaliyopatikana hadi sasa ni ni yale yaliyojengwa Viwanda Kigamboni jijini Dar es salaam pamoja na Mkoani Tanga ,huku akibainisha kupatikana kwa miradi ya kisasa takribani sita yenye hadhi ya kimkakati, ambayo tayari imesajiliwa na kituo hicho na kupitishwa na baraza la Taifa la Uwekezaji.
Miradi hiyo kwa pamoja inategemewa kuwekezwa kwa kiasi cha zaidi ya dola za kimarekanai bilioni 2.626, hali itakayochochea kuongezeka kwa mitaji ya ndani yaani FDI na DDI,pamoja na kuzalisha nafasi za ajira 13,885 ambazo zitawanufaisha zaidi watanzania.
Hata hivyo amebainisha kuwab kuanzia mwezi January hadi julai mwaka huu miradi iliyosajiliwa ni 206 huku sekta ya viwanda ikiongoza kwa kuwa na miradi 118 ,ikifuatiwa na sekta ya utalii na makampuni ya Usfirishaji.
Post a Comment