DODOMA YAPATA HESHIMA NYINGINE KUTOKA KWA WAHANDISI
Bodi ya usajili wa Wahandisi imewasihi waajiri katika sekta mbalimbali za umma na binafsi kuwaruhusu na kuwafadhili wahandisi wao katika Siku ya Wahandisi inayotarajiwa kufanyika Septema 7 na 8 mwaka huu mjini Dodoma.
Akizungmza na wanahabari Kaimu Msajiri wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Patrick Barozi amesema kuwa maadhimisho hayo ni ya 15 tangu kuanzishwa kwa Jumuia ya Wahandisi Januari 13,2013,ambapo maadhimisho hayo yana malengo ya kuwawezesha wahandisi kuonyesha yale wanayoweza kufanya kwa maendeleo ya nchi.
Aidha Barozi maeendelea kusema kuwa maadhimisho hayo yatambatana na maonyesho mbalimbali ya biashara na kiufundi pamoja na mijadala ya kitaaluma,ambapo mada kuu itakayozungumziwa ni Mchango wa Sayansi,Teknolojia,Uhandisi na Hisabati katika kuendeleza viwanda nchini.
Post a Comment