ZIARA YA CHAMA CHA ADC KWA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM
Chama Cha Alliance For Democratic Change (ADC) kimeadhimisha miaka mitano tangu kuanzishwa kakwe kwa kutembelea ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.
Katibu Mkuu wa Chama hicho Doyo Hassan Doyo ameyasema hayo mapema leo hii wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam na kueleza kuwa wamefarijika kwa kupokewa vizuri katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa japokuwa hawakumkuta.
Pia amefafanua kuwa katika maadhimisho hayo watatembelea taasisi mbalimbali, magereza,mahabusu ya watoto, Hospitali ya Taifa Muhimbili kwenda kutoa damu na viomgozi wa dini.
“katika msafara huu nimeambatana na wajumbe zaidi ya 14 wakiwemo Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama,Kamishna Mkuu wa Makao Makuu, Mwenyekiti wa Katiba na Sheria wa chama, Mwenyekiti wa Taifa wa Vijana,Mkurugenzi wa Habari, Wazee wa chama na maafisa mbalimbali”,amesema Doyo.
Hata hivyo chama cha ADC wameomba kwa kipindi hiki cha miaka mitatu iliyobaki Mhe Rais aweze kuwaruhusu kufanya mikutano ya kisiasa iliwaweze kukuza demokrasia na kuongeza wanachama kwani chama hicho hakina mbunge wala diwani.
Aidha chama cha ADC kinatarajia kuanza ziara kwa kutembelea vyombo mbalimbali vya habari hapo kesho mpaka tarehe 30 ya mwezi huu.
Post a Comment