MARUFUKU KUINGIZA ,KUCHINJA NGURUWE MJI WA KIBAHA
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
HALMASHAURI ya Mji wa Kibaha ,mkoani Pwani imepiga marufuku uingiaji na uchinjaji wa nguruwe ili kukabiliana na ugonjwa wa homa ya nguruwe African Swine Fever,ambao unadaiwa kuingia .
Tangu ugonjwa huu uingie jumla ya nguruwe 71 wameshakufa na baada ya kufanyiwa uchunguzi wa awali kupitia dalili za wanyama hao na kwa wale waliokufa viashiria vilionyesha ni ugonjwa huo.
Ofisa Habari wa Halmashauri ya Mji wa wa Kibaha ,Innocent Byarugaba alipozungumza na gazeti hili alisema halmashauri hiyo pia imezuia kuingiza nguruwe .
Byarugaba alieleza ugonjwa huo uliingia mwanzoni mwa mwezi may kwenye kata mbili za Picha ya Ndege na Viziwaziwa eneo la Mikongeni.
“Wananchi wawe na tahadhali ,ugonjwa huu tayari umesababisha vifo vya nguruwe 71 na baada ya kufanyiwa uchunguzi wa awali kupitia dalili za wanyama hao na kwa wale waliokufa viashiria vilionyesha ni ugonjwa huo,” alisema Byarugaba.
Alisema hatua za awali zilizochukuliwa ikiwemo kuzuia nguruwe kuingia na kutoka katika maeneo yaliyokuwa na viasharia .
“Sampuli mbalimbali za nguruwe waliokufa zilichukuliwa na kupelekwa maabara kuu ya mifugo Temeke Jijini Dar es Salaam kwa uchunguzi na kubaini uwepo wa ugonjwa huo ,” alisema Byarugaba.
Hata hivyo ugonjwa wa African Swine Fever,ambao unadaiwa kuingia kwa nguruwe hauwezi kuambukiza binadamu ila madhara yake makubwa ni kuteketeza nguruwe wengi asilimia 100,kwa muda mfupi na kusababisha hasara kwa mfugaji.
Byarugaba alitaja dalili za ugonjwa huo ni kuvuja na kusambaa kwa damu kwenye viungo vya mwili , homa kali, kupumua kwa shida, kutapika, vifo ndani ya siku mbili hadi 10 na muonekano wa damu kuvilia kwenye viungo mbalimbali vya ndani vya nguruwe baada ya kumpasua.
Alieleza kufuatia ugonjwa huo ,idara ya mifugo na uvuvi katika halmashauri ya mji wa Kibaha ,wataalamu wake inatoa elimu kwa wafugaji ili kudhibiti,kwa kupita kata na mitaa .
Ugonjwa huo hushambulia nguruwe na hauna tiba kwa wanyama wanaoupata na husababisha vifo vingi unapotokea hasa kwa wanyama wakubwa.
Post a Comment