IGP SIRO AKAA NA WAZEE WA KIBITI MKOA WA MPWANI NA KUAHIDI KUKOMA KWA MAUAJI KATIKA WILAYA HIYO
Jeshi la polisi nchini limewataka wakazi wa wilaya ya kibiti mkoa wa pwani kuendelea kutoa taarifa ya waharifu kwa jeshi la polisi na kuwaruhusu kuendelea na shughuli zao za kawaida kwa muda wote isipokuwa pikipiki zifanye kazi
mwisho 12jioni, wilayani humo kwani ndiyo chanzo kimoja wapo cha uhalifu katika maeneo hayo
Hayo yamesemwa Leo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Nyakoro Siro alipofanya ziara wilayani humo na kuzungumza na wazee wa eneo hilo ambapo amesema kuwa kwa sasa wako kwenye hatua nzuri katika kupambana na waharifu hao
Aidha IGP amesema kuwa jeshi la polisi limejipanga vyema katika kutokomeza uhalifu na mauaji wilayani kibiti mkoani pwani kwa kushirikiana na wananchi wa wilaya hiyo na kuwatoa hofu wakazi wa wilaya hiyo na kuwaahidi kuwa haitachukua muda mrefu waharifu wote watakuwa wamepatikana kwani wameshapata taarifa zote.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni amesema wako kwenye hatua nzuri kuendelea kuwatafuta waharifu na wanaendelea na jitahada mbali mbali ikiwemo kuzungumza na wazee,viongozi wa dini wa sehemu hiyo.
Na James Bayachamo-Salvanews
Post a Comment