Header Ads

header ad

HUMPHREY POLEPOLE AMPONGEZA RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI KWA KUSIMAMIA RASIRIMALI ZA TAIFA


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akizungumza na wahandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.Picha na Said Khamis
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akizungumza na wahandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Chama Cha Mapinduzi kimewataka viongozi waliotajwa katika taarifa mbili za uchunguzi wa Mchanga wa Madini kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kwa kuwa wamelisababishia Taifa hasara kubwa ya Matrilioni ya Fedha, kutokana na Mchanga wa Madini kwenda nje ya nchi.
          Mbali na hilo Chama kimesisitiza kuwa hakitasita kuchukua hatua kwa wanachama wake iwapo watabainika kuliingizia Taifa hasara kupitia Mchanga wa Madini, ila kwa sasa kinaviachia kwanza vyombo vya dola vifanye kazi yake ya kuwahoji waliotajwa kwenye ripoti hizo mbili.
          Akizungumza na Waandishi wa Habari Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi HAMPHREY POLEPOLE, amesema CCM imetoa pongezi za dhati kwa Rais MAGUFULI ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kwa hatua yake ya uthubutu wa kusimamia raslimali za Taifa.
          POLEPOLE amesema katika Histori ya nchi hatua zilizochukuliwa na Rais MAGUFULI hazijawahi kuonekana popote, hivyo inashangaza kuona baadhi ya Wanasiasa wanakejeli hatua hizo za kishujaa zilizochukuliwa na Kiongozi wa nchi.
          Pamoja na mambo mengine, POLEPOLE, amesema kilichofanywa na Rais MAGUFULI ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo imeelekeza kukomesha wizi unaofanywa na baadhi ya Wawekezaji katika Migodi ya Madini hapa nchini.
          Hata hivyo, CCM kimepongeza hatua za awali zilizooneshwa na Mmliki wa Kampuni ya Barrick Gold Cooparation  kwa kukiri kukosea na kuahaidi kufanya mazungumzo na serikali ili kulipa kiasi cha pesa kinachodaiwa mara watakachokubaliana baada ya mazungumzo na Tanzania.

No comments

Powered by Blogger.