KIKUNDI CHA '' ULIPO TUPO" CHA MWANZA CHAFANYA USAFI KITUO CHA AFYA BUZURUGA
Wanachama wa Kikundi cha Maendeleo (Kikundi cha kusaidia jamii katika masuala mbalimbali) cha ULIPO TUPO cha Buzuruga Jijini Mwanza wakifanya usafi katika Kituo cha Afya Buzuruga jana April 16,2016.
Mwenyekiti wa Kikundi hicho Ndaisaba Aron, amesema uamuzi wa kufanya usafi katika kituo hicho umetokana na msukumo wa uwajibikaji katika jamii unaolenga kuondoa changamoto zinazoweza kujitokeza ikiwemo magonjwa ya milipuko ikiwa wanajamii hawataweza kuwajibika.
"Tumeanzia na eneo jirani, lakini tutakwenda katika maeneo mengine kwa ajili ya kufanya shughuli za maendeleo ambazo pengine serikali ingetoa pesa kwa ajili ya kuwalipa watu ambao wangefanya shughuli hizi, ila kwa kuwa sisi tunajitoa kwa ajili ya shughuli za maendeleo, pesa hizo zitakwenda kufanya shughuli nyingine mhimu katika jamii". Amesema Aron.
Hidaya Bashiru ambae ni mwanachama wa kikundi hicho pamoja na Sixtus Ijugo ambae ni Katibu, wamewasihi wananchi wengine kuwa na desturi ya kushiriki katika shughuli za kijamii ikiwemo katika maeneo mbalimbali kama hospitali, shule na kwingineko kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe.
Diwani wa Kata ya Buzuruga, Richard Machemba, alijumuika na Kikundi hicho kwa ajili ya kufanya usafi katika Kituo hicho cha Afya Buzuruga ambapo amepongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na wakazi pamoja na vikundi mbalimbali vya maendeleo katika Kata yake ambapo amewasihi wananchi kuendelea kujitoa kwa ajili ya kushiriki shughuli za maendeleo.
Eneo hili lilikuwa hatarishi kutokana na baadhi ya wa waharifu kukimbilia huku baada ya kutenda uharifu ikiwemo kupora simu na fedha.
Eneo hatarishi katika eneo la Kituo cha Afya Buzuruga likisafishwa na wanachama wa Kikundi cha Ulipo Tupo cha Buzuruga.
Wanachama wa Kikundi cha Maendeleo (Kikundi cha kusaidia jamii katika masuala mbalimbali) cha ULIPO TUPO cha Buzuruga Jijini Mwanza wakifanya usafi katika Kituo cha Afya Buzuruga jana.
Diwani wa Kata ya Buzuruga nae alishiriki zoezi hilo
Wanachama wa Kikundi cha Maendeleo (Kikundi cha kusaidia jamii katika masuala mbalimbali) cha ULIPO TUPO cha Buzuruga Jijini Mwanza wakifanya usafi katika Kituo cha Afya Buzuruga jana.
Mwenyekiti wa Kikundi hicho Ndaisaba Aron
Mwenyekiti wa Kikundi hicho Ndaisaba Aron, akizungumza na BMG, baada ya kushiriki zoezi la usafi katika kituo cha Afya Buzuruga
Sixtus Ijugo ambae ni Katibu wa Kikundi akizungumza na BMG.
Hidaya Bashiru ambae ni mwanachama wa kikundi hicho akizungumza na Mwandishi wa habari
Diwani wa Kata ya Buzuruga, Richard Machemba akizungumza baada ya kushiriki zoezi la usafi katika kituo cha Afya Buzuruga.
Kituo cha Afya Buzuruga, Kilichopo Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza kikiwa katika hali ya Usafi baada ya Kikundi cha ULIPO TUPO, kufanya usafi.
Post a Comment