Header Ads

header ad

DC IlALA AWAONYA WENYEVITI WA MITAA WATAKAOKWAMISHA WANANCHI KULIPA KODI



MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, amesema hatawafumbia macho wenyeviti wa Serikali za Mitaa watakaokuwa kikwazo cha wananchi kulipa kodi za
majengo kwa kuwa jambo hilo si la kisiasa.

Aidha, Wenyeviti wa serikali za mitaa katika wilaya hiyo wamekubali mamlaka ya ukusanyaji wa kodi za majengo kukabidhiwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuwa itasaidia katika kukusanya kiwango sahihi.

Akizungumza wakati wa kufungua semina ya siku moja kwa wenyeviti wa serikali za mitaa, Watendaji wa Kata na mitaa, Mkuu huyo wa wilaya alisema, suala la ukusanyaji wa kodi si jambo la kisiasa bali ni kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wote.

Akizungumzia semina hiyo, Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Manispaa ya Ilala, Ubaya Chuma, alisema wanaamini hatua hiyo kwa sasa itasaidia kwa kuwa yapo mambo ambayo yamerekebishwa.

Kwa upande wake, Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani, Yusuf Salum Yusuf, alisisitiza kuwa kwa sasa fedha zitakazokuwa zikikusanywa zitaerejeshwa kwa wakati ili mitaa iweze kufanya maendeleo yake.

Alisema kwa mwaka 2015/16 walikuwa na lengo la kukusanya Sh bilioni 7.82 lakini kwa mwaka huu wa fedha 2016/17 lengo lao ni kukusanya Sh bilioni 12.5, ambayo ni ongezeko la asilimia 55.

No comments

Powered by Blogger.