*ASASI ZA KIRAIA WAUNGA MKONO CCM MPYA NA JUHUDI ZA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI.*
Leo Tarehe 10/05/2017 Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi Ndg.Humphrey Polepole Amekutana na kufanya Mazungumzo na Asasi zote za kiraia katika Ofisi ya Kituo Cha Sheria na Haki za Binaadam Dar es salaam.
Ndg.Humphrey Polepole ametumia nafasi hiyo kuwaeleza Asasi za Kiraia dhamira njema ya Serikali, Mageuzi Makubwa yanayofanywa na Chama Cha Mapinduzi pamoja kufafanua Mambo mtambuka.
Asasi za kiraia wakiongozwa na kituo cha Sheria na Haki za Binaadam wameahidi ushirikiano wa kutosha kwa serikali ya Chama Cha Mapinduzi, na Pia Asasi za kiraia wametumia fursa hiyo kuomba nafasi ya kuonana na Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli ili wazungumze naye.
Chama Cha Mapinduzi kwa sasa kinaonekana kuwa karibu na Makundi Mbalimbali na kuwasikiliza na kutatua Changamoto zao. CCM Mpya inaonekana kwa vitendo kwa sasa.
Post a Comment